IDARA YA MIPANGOMIJI:
Idara ya Mipangomiji Manispaa ya Kinondoni imejumuisha Vitengo vifuatavyo:-Mipangomiji, Uthamini, Ardhi, na Upimaji na Ramani na Mali Asili.
Mipangomiji inayo majukumu mawili makubwa ambayo yamegawanyika kama ifuatavyo:-
•Kupanga (Planning and Design)
•Kusimamia Maendeleo ya ukuaji wa mji (Development control)
1.Kuwe na Mchoro wa Mipangomiji unaoainisha matumizi ya ardhi ya viwanja
2.Kiwanja kiwe kimepimwa na upimaji kuidhinishwa na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi
3.Mwombaji atachukua fomu za maombi ya kumilikishwa ardhi kutoka ofisi ya Afisa Ardhi wa Manispaa
4.Mwombaji atajaza fomu hizo atatakiwa kuziwasilisha zikiwa zimejazwa vizuri na aziambatanishe na Mchoro wa Mipangomiji na Ramani ya Upimaji wa kiwanja husika
1. Mwombaji aandae michoro ya usanifu majengo (Architectural drawings) ya jengo analokusudia kujenga. NB: Kwa viwanja vyenye hati miliki, ujenzi unaokusudiwa uzingatie masharti ya uendelezaji yaliyoandikwa kwenye hati ya umiliki wa kiwanja
2. Kwa majengo ya ghorofa mwombaji atatakiwa kuandaa na kuwasilisha michoro ya vyuma ya jengo kusudiwa (structural drawings)
3. Mwombaji atatakiwa kuandika na kuwasilisha barua ya maombi yakibali cha ujenzi kwa Mkurugenzi wa Manispaa
4. Mwombaji atawasilisha michoro yake akiambatanisha na nakala ya hati miliki ya kiwanja katika ofisi ya Msanifu majengo wa Manispaa na atapatiwa fomu maalum za kujaza na baadae atafunguliwa jalada la maombi yake.
5.Kwa maeneo ambayo hayajapimwa (unplanned areas), mwombaji atatakiwa kupitia hatua na. 1-3 hapo juu.
6.Kujaza fomu maalum ya maombi ya kibali cha ujenzi katika maeneo yasiyopimwa.
7.Kuwasilisha michoro ya majengo iliyoandaliwa ikiambatanishwa na fomu maalumu liyojazwa vizuri na Mchoro wa mipangomiji wa eneo husika.
1. Kuandika na kuwasilisha barua ya maombi ya kubadili matumizi ya Ardhi.
2. Barua iambanishwe na vitu vifuatavyo:-
a. Nakala ya hati/barua ya toleo.
b. Ramani ya michoro wa mipangomiji au (extract).
c. Ramani ya upimaji (kwa wale wenye offer pekee).
d. Nakala za risiti za malipo ya kodi ya ardhi.
e. Nakala za risiti za malipo ya kodi ya jengo kwa viwanja vilivyoendelezwa.
f. Michoro ya msanifu majengo (architectural drawings).
g. Nakala ya bango.
Bonyeza hapa kupata mfano wa bango la tangazo la kusudio la kubadili matumizi ya ardhi.
Bonyeza hapa kupata fomu ya maombi ya kibali cha ujenzi kwa maeneo yaliyopimwa.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.