• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fukwe na Visiwa
    • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Matukio ya Utalii
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Iliyopangwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Habari
    • Matukio

Wazo

HISTORIA FUPI:

Kata ya Wazo ni Kata ambayo ilizaliwa na Kata ya Kunduchi. Kwa kipindi hicho Kata ya Kunduchi ilikuwa inaundwa na mitaa sita (06) ambayo ni Tegeta, Wazo Madale, Mtongani, Ununio na Salasala.
Mnamo mwaka 2009 Kata ya Kunduchi ikagawanyika na kuzaliwa Kata ya Wazo. 

Jina la Wazo lilitokana na uwepo wa kiwanda cha saruji (WAZO HILL -TWIGA CEMENT) na watu wengi walikuwa wakifanya kazi katika kiwanda hicho na hapo ndipo jina la Wazo likazaliwa. Kwa kipindi hicho Kata ya Wazo ilikuwa inaundwa na Mitaa sita ambayo ni Salasala, Wazo, Madale, Mivumoni, Kilimahewa na Kisanga. Ilipofika mwaka 2014 Kata ya Wazo iliongezewa mitaa miwili ambayo ni Nyakasangwe na Kilimahewa juu.


ASILI YA WATU WA WAZO; Kabla ya mgawanyiko wa Kata ya Kunduchi na Wazo asilimia kubwa ya eneo la Wazo lilikuwa ni mashamba na mapori na wenyeji wengi walikuwa ni wakulima na wafugaji. Wafanyakazi wachache ni waliokuwa wakifanya kazi kiwanda cha saruji cha Twiga pamoja na wavuvi. Kuna mchanganyiko wa makabila mbalimbali ndani ya Kata ya Wazo ikiwemo, Wamakonde, Wazaramo, Wangoni, Wahehe, Wamwera n.k.


ASILI YA JINA LA MTAA MADALE; zamani Madale ilikuwa ikijulikana kama Madala kwa lugha ya King’indo ikimaanisha kuwa ni sehemu iliyokuwa na tabu, pagumu kuishi. Miaka ya 1980/1990 kulikuwepo na kambi ya SCOUT iliyoanzishwa na Marehemu Hayati Rashid Mfume Kawawa. Bahati mbaya wafadhili waliokuwa wanawafadhili vijana wa kambi hiyo wazungu kutoka Norway walikuwa wanashindwa kutamka neno Madala badala yake wakawa wanatamka Madale. Kwa hiyo majina yote mawili yakaendelea kutumika mpaka mwaka 2014 jina la Madala likafa na Kiserikali likabaki Madale.


IDADI YA MITAA:

Kata ya Wazo ina jumla ya Mitaa nane (08) kama ifuatavyo:-

1.    Mtaa wa Salasala

2.    Mtaa wa Kilimahewa

3.    Mtaa wa Kilimahewa Juu

4.    Mtaa wa Wazo

5.    Mtaa wa Kisanga

6.    Mtaa wa Mivumoni

7.    Mtaa wa Madale

8.    Mtaa wa Nyakasangwe


HALI YA ELIMU:

Hali ya elimu katika Kata ya Wazo ni ya wastani.


SHULE ZA MSINGI ZA SERIKALI:

Kata ya Wazo inazo shule tano (05) za msingi za serikali ambazo ni :-

  1. Shule ya Msingi Salasala
  2. Shule ya Msingi Benaco
  3. Shule ya Msingi Kisauke
  4. Shule ya Msingi Wazo
  5. Shule ya Msingi Nyakasangwe

Kata pia ina shule za  awali na msingi za binafsi 15.


SHULE ZA SEKONDARI ZA SERIKALI:

Kadhalika Kata ya Wazo inazo pia shule tatu (03) za sekondari ambazo ni za Serikali kama ifuatavyo:-

  1. Shule ya sekondari ya Twiga
  2. Shule ya sekondari ya Kisauke
  3. Shule ya sekondari ya Maendeleo.

Kata pia ina shule za sekondari za binafsi 14.


VYUO VYA ELIMU YA JUU NA KATI:

Kata ya Wazo ina chuo  kimoja  cha serikali ambacho ni KMC Vocational Training Centre kilichopo mtaa wa  Mivumoni pamoja  na chuo binafsi  cha Amazon College.


HALI YA AFYA:

Hali ya Afya katika Kata ya Wazo ni ya kuridhisha kwani ina Zahanati na Vituo vya Afya vya serikali na binafsi.


VITUO VYA AFYA VILIVYOPO KATA YA WAZO:

Vituo vya Afya vilivyopo ni viwili (02) ambavyo ni vya binafsi kama ifuatavyo: -

  1. Rabininsia 
  2. Kitengule


ZAHANATI ZILIZOPO KATA YA WAZO:

Zahanati zilizopo katika Kata ya Wazo ni saba (07) ambazo tatu (03) kati ya idadi tajwa ni za serikali na nne (04) ni za binafsi kama ifuatavyo: -

  1. Zahanati ya Salasala - Serikali
  2. Zahanati ya Madale - Serikali
  3. Zahanati ya Wazo - Serikali
  4. Zahanati ya EES - Binafsi
  5. Zahanati ya Arafa - Binafsi
  6. Zahanati ya New Life - Binafsi
  7. Zahanati ya Taifo - Binafsi


HALI YA MIUNDOMBINU:

Kata ya Wazo inayo miundombinu ya barabara za lami na changarawe kuu nne ambazo ni; 

  1. Barabara ya kutoka Madale hadi Kibaoni Mbuyuni yenye urefu wa kilomita 2.5,  
  2. Barabara ya Mbuyuni hadi mwisho w lami yenye urefu wa kilomita 0.3
  3. Barabara ya Afrikana hadi shule ya msingi Salasala yenye urefu wa kilomita 2.5
  4. Barabara ya Skanska hadi IPTL yenye urefu wa kilomita 1.5


MAHUSIANO YA WADAU:

Kata ya Wazo pamoja na wananchi wake inayo mahusiano ya kuridhisha  na wadau wake, na ndio maana wanashirikiana kwa pamoja katika kusukuma maendeleo ya Kata yao.


MIRADI YA KUJIVUNIA KATIKA KATA

  1. Ujenzi wa Kituo cha polisi ghorofa moja - Mtaa wa Madale kwa nguvu za wananchi.
  2. Ujenzi wa daraja la Mbopo
  3. Uwepo wa maabara katika sekondari zote tatu
  4. Uwepo wa Zahanati tatu katika Kata

Matangazo

  • KUFUTA TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI March 14, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA March 13, 2023
  • TANGAZO KWA WASIOLIPIA VIWANJA BOKO DOVYA (KWA SOMJI) NA SALASALA February 15, 2023
  • MABADILIKO YA SIKU YA MAFUNZO YA WASIMAMIZI WA MAUDHUI, WASIMAMIZI WA TEHAMA NA MAKARANI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 July 28, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • JAPAN YAIPATIA MSAADA MZIMUNI SEKONDARI

    March 15, 2023
  • VIKUNDI VYAASWA MATUMIZI SAHIHI YA MIKOPO

    February 18, 2023
  • "HAKUNA TIMU KUBWA ZAIDI YA KMC FC"

    February 18, 2023
  • ULINZI NI KIPAUMBELE KINODONI-DC SAAD

    February 12, 2023
  • Tazama zote

Picha Jongefu

VIKUNDI VILIVYOSEPA NA BILIONI 11 VYAKALIWA KOONI MANISPAA YA KINONDONI. REJESHENI...
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • TARATIBU ZA KUPATA KIBALI CHA UJENZI
  • TAARIFA KWA UMMA
  • RATIBA YA MSTAHIKI MEYA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255 22 2170173

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.