Wakazi wa Kata ya Mbweni, Manispaa ya kinondoni, wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya, Mh. Saad mtambule wameadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika kwa Kupanda Miti zaidi ya 1200.
Katika Hafla hiyo ya Upandaji Miti wakazi wa Kata hiyo wakiambatana na Viongozi mbalimbali wameweza kupanda Miti hiyo katika Mtaa wa Malindi Estate ili kuendelea kulinda Hali ya Mazingira
Pia Mkuu wa Wilaya ameendelea kusisitiza wananchi kutunza mazingira na kuweka Utaratibu wa kupanda Miti katika maeneo yote ya Wilaya ya Kinondoni ili kuunga mkono juhudi za Mh. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan za Nishati safi inayoenda sanjali na utunzaji wa mazingira.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.