Eneo la Kata ya Mbezi Juu hapo awali lilikuwa ni eneo ambao lilikuwa shamba la Mkonge na wakazi wake wengi walitokana na kabila la Wamakonde.
Asili ya jina la Mbezi Juu limetokana na jiografia yake ambayo ni ya milima na mabonde na hivyo kupelekea madhari yake kuonekana kuwa juu sana.
Kata ya Mbezi Juu imetoka kwenye ubavu wa eneo la Kawe ambapo mwaka 2009 iligawanywa na kupatikana Kata ya Mbezi Juu. Kata hii inakadiriwa kuwa na wakazi takribani 41,821
Kata ya Mbezi Juu ilizaliwa kutokana na mgawanyo wa Kata ya Kawe ambayo iligawanywa Mwaka 2009 hatimaye Kata ya Mbezi Juu ikapatikana. Kata ya Mbezi Juu upande wa Kasikazini imepakana na Kata ya Wazo, upande wa Magharibi imepakana na Goba-Ubungo, upande wa Mashariki imepakana na Kata ya Kawe, upande wa Kusini imepakana na Kata ya Makongo.
Idadi ya Watu
Kwa mjibu wa Taarifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, Kata ya Mbezi Juu ina jumla ya Watu 51485, ambapo Wanaume ni 24336, na Wanawake ni 27149.
Mitaa
Kata ya Mbezi Juu ina jumla ya Mitaa Mitano *(5) ambayo ni
-Mtaa wa Jogoo
-Mtaa wa Ndumbwi
-Mtaa wa Mbezi Juu
-Mtaa wa Mbezi Kati
-Mtaa wa Mbezi Mtoni.
Hali ya Elimu
Shule za Awali/Msingi
Kata ya Mbezi Juu ina jumla ya Shule 6 za Awali/Msingi, kati ya hizo 2 ni za Serikali na 4 ni za Taasisi Binafsi.
Shule za Msingi za Serikali
Shule ya Msingi Ndumbwi yenye jumla ya Wanfunzi 1788 kati ya hao Wavulana ni 898 na Wasichana ni 892, Kadhalika Shule hiyo ina jumla ya Walimu 30 Wanaume wakiwa 03 na Wanawake wakiwa 27.
Shule ya Msingi Mbezi Juu ina jumla ya Wanafunzi 1383, Wavulana wakiwa 724 na Wasichana ni 659. Walimu katika Shule hiyo ni 25 ambao wanahusisha Wanaume 6 na Wanawake 19.
Shule za Awali/Msingi Binafsi
Shule ya Msingi Mount Kibo, ambayo ina jumla ya Wanafunzi 999 kati ya hao Wavulana ni 485 na Wasichana wapo 514. Aidha Shule hiyo ina jumla ya Walimu 72 Wanaume wakiwa 25 na Wanawake wakiwa 47.
Shule ya Msingi Kilimani, ambayo ina Wanafunzi wapatao 1618, kati yao Wavulana ni 774 na Wasichana ni 844. Kadhalika Shule hiyo ina jumla ya Walimu 44, Wanaume ni 23 na Wanawake ni 21.
Shule ya Msingi St. Marrys, Shule hii ina jumla ya Wanfunzi 1320, Wavulana wakiwa 673 na Wasichana wakiwa 647, Kadhalika Shule hii ina Walimu wapatao 58 huku Wanaume wakiwa 18 na Wanawake ni 40.
Shule ya Msingi Penuel Mwanzo, Shule hii ina jumla ya Wanafunzi 168 kati ya hao Wavulana wapo 86 na Wasichana wakiwa 82. Walimu waliopo katika Shule hii ni 13 Wanaume wakiwa 5 na Wanawake wakiwa 8.
Shule za Sekondari
Kata ya Mbezi Juu ina jumla ya Shule 5 za Sekondari, ambapo 1 ni ya Serikali na 4 ni za Taasisi Binafsi.
Shule ya Sekondari-Serikali.
Shule ya Sekondari Mbezi Juu
|
Wanafunzi
|
Jumla
|
Walimu
|
Jumla
|
||
Me
457 |
Ke
539 |
996
|
Me
4 |
Ke
18 |
22
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Shule za Sekondari-Binafsi
St Marrys Sekondari
|
Wanafunzi
|
Jumla
|
Walimu
|
Jumla
|
||
Me
208 |
Ke
176 |
384
|
Me
15 |
Ke
14 |
29
|
|
Mbezi Beach Sekondari
|
Wanafunzi
|
Jumla
|
Walimu
|
Jumla
|
||
Me
307 |
Ke
283 |
590
|
Me
41 |
Ke
4 |
45
|
|
Laureate International
|
Wanafunzi
|
Jumla
|
Walimu
|
Jumla
|
||
Me
60 |
Ke
79 |
139
|
Me
15 |
Ke
6 |
21
|
|
Braeburn Dar International
|
Wanafunzi
|
Jumla
|
Walimu
|
Jumla
|
||
Me
23 |
Ke
28 |
51
|
Me
4 |
Ke
3 |
7
|
Maendeleo ya Jamii
Kata ya Mbezi Juu kama zilivyo Kata zingine inao wanufaika wa 10% ya Mikopo inayotolewa na Serikali ikiwa na jumla ya Vikundi 332 ambavyo vyote Wanachama wake ni wanufaika wa mkopo wa 10% usiokuwa na riba.
Aidha Vikundi hivyo vyote vilipata mkopo wa kiasi cha Tsh 1,442,887,000/= kiasi hicho ni tangu mikopo ya 10% ilipoanza kutolewa.
Idadi ya Maafisa Ngazi ya Kata
Kata ya Mbezi Juu ina Maafisa Ugani 13 katika mchanganuo ufuatao;
-Mtendaji Kata 01
-Watendaji wa Mitaa 05
-Maafisa Afya 02
-Afisa Maendeleo ya Jamii 01
-Afisa Kilimo 01
-Afisa Mifugo 01
-Afisa Ustawi wa Jamii 01
-Polisi Kata 01.
Hali ya Afya katika Kata
Hali ya Afya katika Kata inaridhisha, Zahanati zilizopo ni 04, hakuna Kituo cha Afya na kuna Hospitali 01 kwa mchanganuo ufuatao;
Zahanati za Serikali
Zahanati ya Ndumbwi ambayo ina jumla ya Matabibu 08 Wanaume wakiwa 02 na Wanawake 06
Zahana za Binafsi
ONSET GROUP
|
Matabibu
|
Jumla
|
|
Me
03 |
Ke
04 |
07
|
|
KETO
|
Matabibu
|
Jumla
|
|
Me
05 |
Ke
02 |
07
|
|
MICO
|
Matabibu
|
Jumla
|
|
Me
01 |
Ke
01 |
02
|
Hospitali
Kata ya Mbezi Juu ina Hospitali Moja ya MASSANA HOSPITAL ambayo ni miliki ya Sekta Binafsi ikiwa jumla Matabibu 102 kati ya hao Wanaume wapo 37 na Wanawake 65.
Hali ya Miundombinu ya Barabara katika Kata.
Kata ya Mbezi Juu ina jumla ya Barabara 111 za Mitaa, ambapo za Lami ni Tatu (03) pia Kata ya Mbezi Juu imepitiwa na Barabara kuu Mbili yaani Barabara ya Bagamoyo na Barabara ya Goba. Mchanganuo wa Barabara za Mitaa;
-Mtaa wa Mbezi Kati 20
-Mtaa wa Jogoo 16
-Mtaa wa Mbezi Juu 11
-Mtaa wa Mbezi Mtoni 38
-Mtaa wa Ndumbwi 26.
Miradi ya Maendeleo
Ujenzi wa Daraja
Ujenzi wa Daraja la Mito miwili Mtaa wa Ndumbwi lenye thamani ya Tsh 450,000,000/= Daraja hili linasimamiwa na TARURA, Ujenzi wake unaendelea na umefikia 90% kukamilika. Chini ya Mkandarasi Southern Link Ltd.(picha)
Ujenzi wa Kivuko
Ujenzi wa Kivuko cha Waenda kwa Miguu Mtaa wa Ndumbwi chenye thamani ya Tsh 23,735,098. Ambacho kipo hatua za awali za kutengeneza mchoro na makadilio. (picha).
Biashara na Uwekezaji
Kata ya Mbezi Juu ina Soko Moja ambalo lipo chini ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni lenye frem za Biashara 50. (picha). Shughuli kuu za Uchumi za Wananchi wa Kata ya Mbezi Juu ni Biashara, Ufugaji na Ajira.
Hali ya Ulinzi na Usalama
Hali ya Ulinzi na Usalama katika Kata ni nzuri sana, hali hii inachagizwa na uwepo wa Vikundi vya Ulinzi na Shirikishi katika kila Mtaa kwa Kata nzima. Aidha Kata ya Mbezi Juu ina Kituo kimoja cha Polisi. Kituo cha Polisi Makonde ambacho kinafanya kazi kwa ukaribu na Vikundi vya Ulinzi Shirikishi kuhahakisha Amani inakuwepo katika Kata.
Hali ya Usafi wa Mazingira
Hali ya Usafi wa Mazingira Kata ya Mbezi Juu ni nzuri, Suala la kuhahakisha takataka hazizagai hovyo lipi chini ya Mkandarasi NIMA GENERAL ENTERPRISES ambaye anatoa ushirikiano thabiti katika uzoaji wa taka za Majumbani na Viwandani, lakini pia Kata ya Mbezi Juu inashirikiana na SUMA JKT ambao wamepewa kazi ya Ukandarasi ya kuhahakisha usafi wa Barabara na Mitaro.
Ushirirkiano na Wadau wa Maendeleo.
Kata ya Mbezi Juu imekuwa na Ushirikiano mzuri na Wadau mbalimbali wa Maendeleo wa ndani ya Kata na hata wale wa nje ya Kata, ambapo wamekuwa mstari wa mbele katika kuchangia shughuli mbalimbali zinazofanywa na Serikali ili kuhakikisha huduma bora inapatikana katika Kata.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.