• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

Mbweni

HISTORIA FUPI:

Kata ya Mbweni ni miongoni mwa Kata 20 za Manispaa ya Kinondoni. Asili ya jina Mbweni ni uwepo wa bandari kubwa ya asili iliyokuwa inatumika na Wareno enzi za ukoloni, jina ambalo wageni na wenyeji walilitumia wakimaanisha ni sehemu tulivu.

Sehemu ya BANDA MOJA, kwa sasa ni MITI 3 kulikuwa na makaburi ya Wahindi, Waarabu na Wasomali ambao wote walifika katika vipindi tofauti eneo la Mbweni kwa ajili ya kupakia na kushusha bidhaa zao kwa kutumia eneo la bandari lilikokuwa likijulikana kwa jina la STAHABUU ambalo kwa sasa kuna kambi ya kijeshi ya 19 (JKT). Uwepo wa bandari hii ulipelekea mji kutanuka haswa maeneo ya Mpiji na Teta.

Mtaa wa Teta ulikuwa na mashamba ya miembe, minazi na mikorosho. Bidhaa mbalimbali zilikuwa zinasafirishwa katika eneo hili zikiwemo vipusa na mchele kwenda Uarabuni kwa kutumia majahazi makubwa.

Eneo ambalo kwa sasa ni Mtaa wa Maputo kulikuwa na shamba enzi za ukoloni na Bagamoyo ilikuwa ni Makao Makuu. Kiongozi mkuu wa eneo hili alkuwa akifahamika kwa jina la GULAMRASSUR na alikuwa ni LALIWI, cheo kama cha Mkuu wa Wilaya (DC) kwa sasa. Kazi yake kubwa ilikuwa ni kusimamia mashamba na wakulima ambao walilazimishwa kulima mazao ya korosho na mihogo.

Mtaa wa Malindi Estate paliitwa MMARANII na palikuwa na jela ya watoto na msikiti ambao ulijengwa na mzungu aliyeitwa BELL ambapo kwa sasa ndio eneo la USALAMA WA TAIFA.

Mitaa

Kata ya Mbweni ina jumla ya Mitaa Mitano (5) ambayo ni; Mbweni, Malindi Estate, Mapatano, Mbweni mpiji na Mbweni teta

  1. Mtaa wa Teta
  2. Mtaa wa Maputo
  3. Mtaa wa Mpiji
  4. Mtaa wa Malindi Estate
  5. Mtaa wa Mbweni

Idadi ya Watu

Kwa mjibu wa taarifa ya Sensa ya Mwaka 2022, Kata ya Mbweni ina jumla ya Wakazi 25970. Katika hao Wanaume ni 12502 na Wanawake ni 13468.

Hali ya Elimu 

Kata ya Mbweni ina jumla ya Shule Kumi na Nne (14) ambazo zinajumuisha Shule za Awali/Msingi na  Sekondari  ambapo kuna Shule 08 za Awali/Msingi, 06 zikiwa chini ya miliki ya  Taasisi Binafsi na 02 zinamilikiwa na Serikali. Shule za Sekondari ni 06 kwa ujumla wake, 04 zinamilikiwa na Sekta Binafsi na 02 ni za Serikali, kati ya Shule mbili zinazomilikiwa na Serikali moja ina kidato cha sita ambayo ni Mbweniteta.

Shule za Awali/Msingi za Serikali

-Mbweni na

-Kiumbageni

Shule za Awali/Msingi za Binafsi

-Hope and Joy

-Kings and Queens

-Mount Evarest

-Shausiye/Feza

Shule za Sekondari za Serikali

-Teta

-Mbweni

Shule za Sekondari za Binafsi

-Hope and Joy

-Shausiye/Feza

Idadi ya Wanafunzi

Hali ya Afya katika Kata

Kata ya Mbweni ina jumla ya Zahanati 02, Vituo vya Afya 03 na Hospitali 01

Zahanati za Serikali 

-Zahanati ya Mbweni

-Zahanati ya Mpiji

Zahanati Binafsi

-Hakuna

Vituo vya Afya vya Serikali

-Kituo cha Afya Malindi

Vituo vya Afya Binafsi

-Armed Health Center

Hospitali za Serikali

-Hakuna

Hospitali Binafsi

-St Joseph Hospital

Miundo mbinu

Kata ya Mbweni ina Barabara Tano (5) za kiwango cha lami zikiwa na urefu wa km 20. Aidha Kata ya Mbweni katika Mitaa yake Mitano (5) ina jumla ya Barabara zipatazo 58.

Biashara na Uwekezaji

Kata ya Mbweni ina soko moja la Biashara la Mpiji, kituo kimoja cha Daladala (mabasi) na Bandari moja ya Mbweni  pamoja na ufukwe wa JKT Mbweni. Uwepo wa vitu tajwa unawapa Wananchi na Wakazi wa Mbweni kujihusisha katika Biashara, Uvuvi na Ajira zikiwa shughuli kuu za Uchumi wao.

Miradi ya Maendeleo

Kata ya Mbweni imekamilisha miradi miwili ya Sekta ya Elimu na Biashara kwa kujenga Shule ya Sekondari ya Teta (picha) na ujenzi wa Soko la Mpiji (picha) ambapo miradi imeshakamilika.

Ulinzi na Usalama

Hali ya ulinzi na usalama ni shwari kabisa katika Kata ya Mbweni ambapo kuna vituo viwili (2) vya polisi cha Maputo na Masaiti lakini pia kila Mtaa wa Kata ya Mbweni kuna kikundi cha ulinzi shirikishi (sungusungu) kwaajili ya kuimarisha ulinzi na usalama wa Mtaa.

Idadi ya Maafisa ngazi ya Kata

Kata ya Mbweni ina Maafisa Ugani wapatao 14 katika mchanganuo ufuatao;

Afisa Mtendaji Kata 01

Watendaji Mitaa 05

Afisa Afya-01

Afisa Maendeleo ya Jamii-01

Afisa Kilimo-01

Afisa Mifugo-01

Afisa Uvuvi- 01

Mratibu Elimu Kata-01

Afisa Usitawi wa Jamii-01

Vivutio vya Utalii

Kata ya Mbweni ina vivutio viwili vya utalii kwa maana ya Bandari na Ufukwe wa JKT Mbweni.



Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.