Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Songoro Mnyonge, Oktoba 25, 2024 ameongoza Hafla ya Kuwaaga Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wa Manispaa ya Kinondoni waliomaliza muda wao wa kuwepo madarakani.
Hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Soko la Magomeni ililenga kuwapongeza na kuwatunuku vyeti vya shukrani kwa wenyeviti hao kwa utumishi wao ndani ya miaka mitano.
Aidha, walipongezwa kwa juhudi kubwa za kuchangia maendeleo katika sekta mbalimbali za Afya, Elimu, Maji, Miundombinu, Mikopo kwa vijana na wanawake pamoja na kuchangia katika ukusanyaji wa mapato ndani ya Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.