WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Mheshimiwa Dorothy Gwajima, amewataka wazazi na walezi kuzungumza mara kwa mara na watoto wao ili kubaini iwapo wanafanyiwa vitendo vya udhalilishaji.
Waziri Gwajima ameyasema hayo alipotembelea shule ya Starlight iliyopo Tegeta, kufuatia watumishi wawili wa shule hiyo kutuhumiwa kumdhalilisha mtoto wa miaka sita.
Alisema, "Ni vizuri wazazi na walezi kuzungumza na watoto, na kama kuna dalili za udhalilishaji taarifa zitolewe mapema."
Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mheshimiwa Godwin Gondwe, alimweleza Waziri Gwajima kuwa tayari watuhumiwa hao wamekamatwa.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini: Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255 22 2170173
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.