• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

WAZAZI BUNJU WAPEWA MAFUNZO YA LISHE KWA VITENDO

Tarehe iliyowekwa: December 22nd, 2023

Wazazi na Walezi kutoka Kata ya Bunju, Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni wametakiwa kuzingatia vyakula vyenye makundi matano wakati wa uandaaji wa vyakula kwa watoto wao.

Hayo yamebainishwa na Afisa Lishe kutoka  Sehemu ya Kilimo na Mifugo Manispaa ya Kinondoni Bi. Luciana Msangi wakati akitoa mafunzo ya lishe na namna ya uandaaji wa chakula hivyo kwa vitendo Disemba 22, 2023 katika Ofisi ya Mtendaji Kata ya Bunju.

Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Ofisi ya Kata ya Bunju ikiwa ni moja ya utekelezaji wa Mkataba uliosainiwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na maelekeo ya Mkurugenzi wa Manispa ya Kinondoni Bi. Hanifa Suleiman Hamza, kwamba kila Kata inapaswa kutoa mafunzo ya lishe kila baada ya miezi mitatu.

"Leo tupo Kata ya Bunju kutoa mafunzo ya lishe na namna ya uandaaji wa vyakula vinavyozingatia makundi matano ya vyakula kama vile vyakula vya mizizi, nafaka, mafuta, mbogamboga na matunda ili kuisaidia jamii kuwa na kizazi chenye afya bora kwani vyakula hivi vinasaidia kuondokana na magonjwa nyemelezi yasiyoambukiza pamoja na  ukuaji mzuri wa watoto," amesema Bi. Luciana.

Aidha Bi. Luciana amewashauri akina mama hao kuwa makini wanapoandaa vyakula vya lishe kwa watoto wao hasa uandaaji wa uji wa lishe wenye mchanganyiko wa nafaka zaidi ya moja ambapo kwa wamama wenye watoto kuanzia miezi 6 wanatakiwa kitumia chakula chenye nafaka aina moja tu kwani mfumo wao wa chakula unakuwa  bado hauwezi kumeng'enya mchanganyiko wa vitu vingi.

Lakini pia Bi. Luciana ameshauri kuwa watoto wenye umri kuanzia mwaka mmoja na kuendelea  wanatakiwa kupewa chakula chenye mchanganyiko wa aina  zisizozidi mbili pamoja na kuongeza virutubishi kama karanga, maziwa,  mbegu za maboga wakati wa kupika uji na sio kuvisaga pamoja kama wengi walivyozoea kwani kufanya hivyo wanatengeneza sumu kavu ambayo sio nzuri kwa watoto bila ya kusahau matunda na mbogamboga.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wenyeviti Wilaya ya Kinondoni Bw. Lazarious Mwakiposa amewasisitiza wamama hao kutokuwa wavivu katika uandaaji wa vyakula ndani ya familia zao ili kuondokana na magonjwa hatarishi yanayosababishwa ulaji usiofaa hasa kwa watoto wao.

Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.