• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

WAVAMIZI ENEO LA KIWANDA CHA KUCHAKATA TAKA MABWEPANDE WATAKIWA KUONDOKA MARA MOJA

Tarehe iliyowekwa: December 14th, 2020

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam Mhe.Abubakar Kunenge leo alipofanya ziara ya ukaguzi wa kiwanda cha kuchakata taka kilichopo Kata ya Mabwepande Manispaa ya Kinondoni.

Amesema eneo hilo enye ekari 14,  lilitengwa kwa ajili ya shughuli za uchakataji wa taka ikiwa ni hatua za Serikali za kuhakikisha inatatua kero za uchafu zinazowakabili wananchi katika maeneo yao, lakini pia ni moja ya kitega uchumi kwa kuzalisha mbolea isiyo na kemikali itakayoweza kuuzwa kwa wanachi na wadau mabilimbali na si kwa ajili ya makazi.

 Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Abubakar Kunenge na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo wakikagua mradi.

"Ninaagiza wale  wote waliovamia eneo hilo kuondoka mara moja ili kuepukana na adha ya kubomolewa na kuharibiwa mali zao na  ninyi Manispaa wekeni mipaka katika eneo hili ili ijulikane mwanzo na mwisho wake.  Nilazima wana Dar es salaam mjifunze kufuata Sheria, kuitii Sheria na si vinginevyo." Ameagiza RC Kunenge.

Katikati ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Songoro Mnyonge

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe.Songoro Mnyonge alipokuwa akitoa ufafanuzi amesema  kiwanda hiki kinachojengwa kwa ufadhili  kutoka jiji la Humburg Nchini Ujeruman, kinauwezo wa kuchukua tani 50 za taka kwa siku na kuzichakata hadi kufika tani 30 kwa siku moja kwa kutumia mitambo ya kisasa itakayofungwa katika eneo hilo.


Amesema mitambo ya kuchakata taka tayari imefika bandarini ikisubiri ukamilishwaji wa taratibu za kiserikali ili iweze kufungwa tayari kwa kuanza kazi.

Akitoa ufafanuzi wa kiwanda hicho, Afisa Usafishaji wa Manispaa hiyo  Ndg Alban Mugyabuso amesema mfumo mzima wa uchakataji taka hadi kukamilika kwake unatumia siku 14, na kwamba tayari masoko yameshaanza kutafutwa kwajili ya ununuzi wa mbolea isiyo na kemikali itakayopatikana baada ya uchakataji.


Aidha ameeleza kuwa takataka zinazochukuliwa kwa ajili ya uchakataji ni zile zinazotoka masokoni zenye kuoza kwa haraka na siyo chupa za maji wala mifuko ya plastiki.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewataka TRA na Bandari kushughulikia kwa haraka mitambo hiyo iliyoko bandarini  iweze kutoka ili ifungwe na kiwanda kiweze kufanya kazi.

Imeandaliwa na

Kitengo Cha Uhusiano na Habari.

Manispaa ya Kinondoni.

Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.