• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

WATOTO TAKRIBANI MILIONI 3.5 DUNIANI WALIO CHINI YA MIAKA MITANO, HUPOTEZA MAISHA KILA MWAKA KWA MAGONJWA YA MLIPUKO IKIWEMO KIPINDUPINDU. .

Tarehe iliyowekwa: November 27th, 2017

 NI KUTOKANA NA KUSHUKA KWA KIWANGO CHA UNAWAJI WA MIKONO KWA USAHIHI KUTUMIA SABUNI NA MAJI YANAYOTIRIRIKA.

 Watoto takribani milioni 3.5 kote uliwenguni hupoteza maisha kila mwaka kutokana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu, na hii ni kutokana na kutokunawa mikono kwa usahihi. 

 Hayo yamebainishwa leo na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Tandale Sokoni Bi. Murshda Ally Kiswela alipokuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Diwani wa Kata hiyo, kwenye mkutano wa mafunzo ya kuongeza uelewa juu ya kuzuia na kujikinga na maambukizi ya magonjwa kwa unawaji sahihi wa mikono, uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi tandale. 

 Amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea watanzania hasa wanafunzi, uwezo na uelewa wa jinsi gani mikono inatakiwa kuoshwa, na kuhakikisha inabaki safi na salama ili kujiepusha na magonjwa hatarishi ya mlipuko yatokanyo na unawaji usio sahihi. 

 "Lengo la mkutano huu wa mafunzo ni kuwajengea uelewa na ufahamu zaidi wa umuhimu wa unawaji mikono kwa kupitia njia kumi kwa maji tiririka na sabuni, na kukausha mikono kwa kitambaa kisafi au tishu ,hii ni njia madhubuti na rahisi katika udhibiti wa magonjwa yanayoweza kusababishwa na mikono iliyochafuka na vimelea vya magonjwa, inadaiwa kwamba magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu yanatokana na unawaji wa mikono usio sahihi, takribani watoto  milioni 3.5 waliochini ya miaka mitano hupoteza maisha kila mwaka duniani kote. "Ameeleza Mwenyekiti

 Naye Dr. Omary Mwangaza ambaye ni mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Magomeni amebainisha kuwa kila siku duniani watoto takribani elfu mbili mia moja tisini na tano(2,195) hupoteza maisha kwa ugonjwa wa kuharisha, na watoto takribani laki mbili na nusu, (250,000), hupoteza maisha kwa ugonjwa wa kipindupindu. 

 Amesema asilimia hamsini ya magonjwa hayo yanayosababishwa na kutokunawa mikono katika jamii ikiwa ni pamoja na kipindupindu, kuhara, kutapika, kuharisha damu, pamoja na Amoeba yatapunguwa endapo njia sahihi za unawaji wa mikono zitafundishwa, kuzingatiwa na kudumishwa. 

 Kadhalika Afisa Afya wa Manispaa hiyo Ngd John Kijumbe ameongeza kuwa Manispaa ya Kinondoni ili kuondokana na magonjwa yanayosababishwa na unawaji wa mikono usio sahihi imepanga kuweka progam pamoja na bajeti ya kutosha kwa idara na vitengo vyote ili iweze kutoa elimu ya unawaji wa mikono kila kata na mashuleni  kwa wakati na usahihi. 

 Katika hatua nyingine Sr. Rose Temu ambaye ni Afisa Muuguzi kituo cha Afya Magomeni ameainisha njia kumi sahihi za unawaji wa mikono kuwa ni kwanza kulowanisha mikono kwa Maji, weka sabuni ya kutosha kiganjani, sugua kiganja kwa kiganja, osha nyuma ya kiganja na safisha vidole kwa kupitanisha. 

 Nyingine ni safisha nyuma ya vidole kwa kukunja vidole, safisha vidole gumba, safisha kucha za mkono mmoja mmoja kwenye kiganja cha mkono mwingine, suuza mikono kwa maji safi, kausha mikono kwa karatasi au kitambaa kisafi, na mwisho funga bomba kwa kiwiko au tishu. 

 Imetolewa na
 Kitengo cha Uhusiano na habari
 Manispaa ya Kinondoni

Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.