Wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye banda la Manispaa ya Kinondoni katika maonesho ya Nane nane ili waweze kupata Elimu ya kutosha kuhusiana na kilimo cha mboga mboga na ufugaji wa kisasa.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Alli Hapi alipohojiwa na waandishi wa habari wakati anatembelea banda la Maonesho katika viwanja vya nane nane vilivyoko Mkoani Morogoro.
Amesema wananchi wasisubiri kuwa na maeneo makubwa ndipo walime, kipo kilimo cha kisasa kinachohitaji eneo dogo, na ukalima Kilimo cha faida kama mboga mboga pamoja na ufugaji.
Ameongeza kuwa sio Kilimo tu, hata usindikaji wa vyakula kupitia mbogamboga za kijani ambapo unaweza ukatengeneza unga kupitia mhogo, na keki kupitia unga wa mchicha nafaka.
Naye Naibu Meya Manispaa ya Kinondoni Mh.George Manyama amesema kilimo ni faida, na kupitia kilimo unaweza ukajikwamua kiuchumi, ukasomesha watoto, ukajenga na kufanya vitu vya maendeleo.
Amewasihi wanachi wajitokeze kutembelea banda la kinondoni wapate elimu ya kutosha kuhusiana na Kilimo bora cha kisasa.
Kueleka nane nane kauli mbiu inasema "Zalisha kwa Tija mazao na bidhaa za Kilimo, mifugo na uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati ".
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.