• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

WAKULIMA KINONDONI WAMETAKIWA KUELEWA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIA NCHI KATIKA SEKTA YA KILIMO ILI WAWEZE KUKABILIANA NAZO

Tarehe iliyowekwa: January 18th, 2019

Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bi.Stella Msofe, alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tatu yaliyoendeshwa katika kituo cha kilimo malolo kwa lengo la kutoa elimu mahususi juu ya mabadiliko ya tabia nchi katika sekta ya kilimo na jinsi ya kukabiliana nayo.

Amesema ni lazima wakulima hawa wapatiwe elimu ya kutosha itakayowawezesha kuepukana na athari hizo, kwani kilimo ndio uti wa Mgongo wa Taifa letu, hasa ikizingatiwa tunahitaji malighafi za kutosha kuendeshea viwanda vyetu,  ambayo kwa sasa ndio sera ya Serikali ya awamu ya tano, Serikali ya viwanda.

Amesema "Bahati nzuri Kinondoni tunayohazina ya wataalam wa sekta hii, tunacho kituo bora kabisa kwa ajili ya elimu hiyo, kwanini tushindwe kutoa elimu kwa walengwa?, kwanini wakulima wetu wasipate elimu, wataalam hawa wapo, na  wanalipwa kwa kazi hiyo, hivyo watumieni, kwani jukumu lao ni kurudisha ujuzi, elimu na maarifa kwa jamii husika." Bi.Msofe.

Awali  akiainisha lengo zima la mafunzo hayo kwa Katibu Tawala huyo,  Mkuu wa Idara ya kilimo na mifugo Manispaa ya Kinondoni, ambaye pia ni   msimamizi wa kituo cha kilimo Malolo,  Bw Salehe Hija amesema, mafunzo haya yaliyohusisha wakulima 40, kutoka Kata tano za Manispaa hiyo, yamelenga si tu kutoa uelewa,  bali pia kuainisha  njia sahihi za kupambana na changamoto zake, ili wakulima waweze kufanya kilimo chenye tija.

Amezitaja Kata zilizoshiriki mafunzo hayo kuwa ni kata ya  Mbweni, Bunju, Mabwepande, Wazo na Kunduchi, na kuwataka wakulima hao kuwa mabalozi kwa wakulima wengine kwa elimu waliyoipata, ili elimu ienee na kuweza kuleta tija.

Akishukuru uongozi wa Manispaa ya kinondoni kwa kuendesha mafunzo hayo,  kwa niaba ya wakufunzi wengine, Mwenyekiti wa wakulima waliopatiwa mafunzo hayo Bw John Malekela  amesema elimu hii ni hazina tosha kwa sekta nzima kwa Wilaya yetu, kwani tunaahidi kuitendea kazi  ili waweze kuepukana na  changamoto hizo za mabadiliko ya tabia nchi na waweze pia kujiongezea thamani ya mazao yao.

Imeandaliwa na

Kitengo Cha Habari na Uhusiano

Manispaa ya Kinondoni.

Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.