Ujenzi wa barabara ya Rashidi yenye urefu wa Km 0.85 umeanza rasmi Mara baada ya kukamilika kwa zoezi la ulipwaji wa fidia kwa wananchi ambao watapitiwa na mradi huo.
Akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo amesema Ujenzi wake ni utekelezaji wa agizo la Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Mhe Chongolo amesema kuwa akiwa msimamizi mkuu wa shughuli za serikali katika wilaya hii amekuja kuangalia maendeleo ya mradi huo na kuona Kama kuna changoto zozote waweze kuzitatua kwa wakati na hivyo kuwezesha mradi huo kukamilika kwa wakati.
Aidha amesema kukamilika kwa mradi huo kutapunguza kero ya mafuriko ambayo yalikua yanatokea katika maeneo hayo msimu wa mvua hapo awali kwani Ujenzi wa barabara hiyo utahusisha Ujenzi wa mifereji mikubwa ya maji itakayosaidia kupeleka maji baharini.
Kwa upande wake Msimamizi wa barabara hiyo toka TARURA Mhandisi Lydia Machibya amesema barabara hiyo itajengwa kwa awamu kwani mchoro wa barabara hiyo unaonesha barabara hiyo inamuunganiko na barabara nyingine, hivyo kwasasa ujenzi utaanza kwa awamu ya kwanza.
"Nyumba 51 zinatakiwa kupisha mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati ambapo baadhi yao tayari wameshaaanza kubomoa nyumba zao wenyewe kwani tayari wameshapata fidia zao" amesema Mhandisi Lidya
Aidha wananchi wanaoishi maeneo hayo wamemshukuru Mkuu wa wilaya ya Kinondoni kwa kuwa nao begakwabega, na kufanya vikao vya marakwamara kupokea maoni ya wananchi katika kuhakikisha ujenzi wa barabara hii unakamilika kwa wakati.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.