Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Bi. Hanifa Suleiman Hamza, amesisitiza kilimo cha matunda na mboga mboga shuleni.
Bi. Hanifa aliyasema hayo Januari 30, 2024 wakati wa Kikao cha Tathmini ya Mkataba wa Lishe Robo ya Kwanza. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Afya, Manispaa ya Kinondoni.
Alisisitiza kuwa, " siridhishwi na hali ya upatikanaji matunda na mboga mboga shuleni," na kutoa rai kuwa, "tuoteshe matunda na mboga mboga."
Aidha, aliwataka Maafisa Kilimo kuwajengea uwezo wanafunzi katika lishe na kilimo na kuelekeza kuwa, "tuwajengee wanafunzi uwezo wa kujitegemea."
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.