Wanawake wa Wilaya ya Kinondoni wameaswa kuthibitisha kauli mbiu ya siku ya Wanawake inayosema "Wekeza kwa Wanawake ili kuharakisha maendeleo na ustawi wa jamii" kwa vitendo.
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni Bi. Stella Msofe katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Kiwilaya yaliyofanyika Machi 13, 2024 katika Uwanja wa Mwinjuma, Kata ya Makumbusho.
Katika maadhimisho hayo Bi. Msofe alishukuru jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuhakikisha Taifa letu lipo kwenye mikono salama chini ya mikono yake na pia katika kuhakikisha anawawezesha wanawake kiuchumi na kuhakikisha wanawake wanakuwa na afya njema.
"Bi. Msofe alisema, "Tunamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha afya ya mama mjamzito iko salama tangu akiwa mjamzito mpaka anapojifungua kwa kuboresha huduma na miundombinu ya sekta ya afya."
Aidha, Bi. Msofe amewaasa wanawake kuthibitisha kauli mbiu ya siku ya Wanawake Duniani kwa kujitokeza kwa wingi katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi nchini.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.