Akitoa tathmini hiyo leo, Afisa elimu msingi Manispaa ya Kinondoni Bw.Kiduma Mageni amesema, jumla ya shule 138, zenye wanafunzi 12, 622, walifanya mtihani huo ambao ni sawa na asilimia 99.33% na kati yake waliofaulu ni 9,302, sawa na asilimia 74.20%
Amesema lengo la mtihani huu ni kutekeleza mkakati maalum wa kuhakikisha inaendelea kufanya vizuri kitaaluma hasa ikizingatiwa Kinondoni ilishika nafasi ya tatu Kimkoa kwa ufaulu wa asilimia 95.70%, matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE) 2018.
"Kinondoni iliandaa mkakati maalumu wa kuendelea kufanya vizuri zaidi kitaaluma kwa kuhakikisha inaendesha mitihani miwili ya utamilifu kiwilaya kwa wanafunzi wa darasa la saba 2019 na mtihani huo ulifanyika tarehe 27-28/03/2019" Amefafanua Mageni.
Aidha amezitaja shule tatu za serikali zilizofanya vizuri kuwa ni Msisiri, Victoria na Lugalo na shule za binafsi ni Royal Elite, Mother's of Mercy na Libermann.
Amewataka walimu kutumia Matokeo haya kama chachu ya kurekebisha changamoto ndogondogo zilizoonekana ili kuweza kufanya vizuri mitihani ijayo ya ngazi ya Mkoa na Taifa.
Katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Oysterbay na kuenda sambamba na ugawaji zawadi kwa shule zilizofanya,vizuri kutoka CRDB Bank, pia imehudhuriwa na waalimu wakuu, waratibu wa Elimu Kata pamoja na waalimu wa darasa la saba.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.