*Vetagro East Africa Limited kwa Kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni Yagawa Mbegu kwa Ajili ya Programu ya Kilimo cha Mbogamboga Shuleni* Leo, Vetagro East Africa Limited imekabidhi mbegu kwa Manispaa ya Kinondoni kwa ajili ya kuendesha programu ya mafunzo ya kilimo cha mbogamboga kwa vitendo katika shule zote za manispaa hiyo. Lengo la programu hii ni kuwaelimisha wanafunzi juu ya mbinu bora za kilimo na kuwapa ujuzi wa vitendo wa kulima na kutunza mazao. Programu hii inalenga kuchochea maendeleo ya kilimo na kuhakikisha kizazi kipya kinaelewa umuhimu wa kilimo endelevu. Hii ni sehemu ya jitihada za kuimarisha sekta ya kilimo katika ngazi ya jamii kwa kuanzia na shule, huku ikilenga kuwajengea wanafunzi misingi imara ya ujuzi wa kilimo.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.