• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

NAIBU WAZIRI OR-UTUMISHI NA UTAWALA BORA AKUTANA NA WATUMISHI WA MANISPAA YA KINONDONI

Tarehe iliyowekwa: December 12th, 2022

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi leo Jumatatu tarehe 12 Disemba, 2022 amekutana na Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni katika kikao kazi cha kusikiliza kero/malalamiko/changamoto za watumishi kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Turiani, uliopo Kata ya Ndugumbi Manispaa ya Kinondoni.Katika kikao hicho Watumishi walipata fursa ya kuelezea changamoto za kiutumishi na kupatiwa ufafanuzi hususani katika maeneo yanayohusu kupandishwa madaraja, kubadilishwa vyeo, madai ya nyongeza za mishahara na malimbizo ya mishahara na yaliyojibiwa vizuri na Naibu Waziri sambamba na kutolea ufafanuzi na kukidhi kiu ya Watumishi.

Akizungumza wakati wa majumuisho ya kikao hicho aliwataka Watumishi wote kutekeleza kwa ufanisi majukumu yao kwa kutoa huduma bora kwa wanachi na kwa wakati kwani Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonyesha mapenzi makubwa kwa watumishi wa umma kwa kulipa malimbikizo ya mishahara  kwa watumishi wa Kinondoni kutoka  Milioni 313  hadi Bilioni 1.7 na kupandisha madaraja watumishi 1,276 katika kipindi kifupi cha utawala wake hivyo amewataka watumishi kuthamini adhima hiyo ya Rais kwa kufanya kazi kwa uhakika, bidii na ufanisi wa kiwango cha juu.

Mhe. Ndejembi amewakumbusha watumishi masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuacha ukirimba, kuacha majungu, usengenyaji kazini, na kuacha kufanya kazi kwa mazoea. 

Pia alisisitiza umuhimu wa kila mtumishi wa umma kuwa na mpango kazi wa siku, wiki, mwezi  na mwaka katika kutoa huduma kwa wananchi utakaowezesha kujitathimini binafsi na kuwaagiza Wakuu wa Divisheni na Vitengo kukutana na watumishi walio chini yao na kusikiliza kero hasa Divisheni ya Utumishi na Utawala.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni Bi. Stella Msofe, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Songoro Mnyonge na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Bi. Hanifa Sulemani Hamza ambapo walimshukuru Naibu Waziri kwa kutenga muda wake kuzungumza na watumishi hao na kumuahidi usimamizi wa karibu kutoka kwao katika kutekeleza maagizo yote aliyotoa katika kikao hicho.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini:

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni 

Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.