• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

MISINGI YA HAKI NA WAJIBU, NDIO NGUZO PEKEE YA MAFANIKIO KWENYE UTUMISHI WA UMMA"

Tarehe iliyowekwa: August 24th, 2018

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,  Mh. Daniel Geofrey Chongolo alipokutana na watendaji wa Kata na Mitaa, pamoja na wakuu wa idara na vitengo,  katika kikao kazi kilichofanyika ukumbi wa Oysterbay shule ya Msingi leo.

Amesema kila, mtumishi wa Umma anao wajibu wa kutekeleza majukumu yake kwa wakati kwa kusimamia misingi ya sheria, kanuni na taratibu , ili kuepukana na migogoro inayoweza kuzuilika kwa mara moja.

"Sisi tukitimiza wajibu wetu, kwenye maeneo yetu, hakuna mtu atakayepeleka malalamiko Wilayani, Mkurugenzi weka utaratibu wa kila mtu kuwa part and parcel ya eneo lake la kazi" Amesisitiza Mh.Chongolo.

Kadhalika, amewataka watendaji wa Kata na Mitaa kuwa mstari wa mbele katika Kuzuia na kuepusha migogoro ya Ardhi, kuwa mstari wa mbele kukusanya mapato, kusimamia maswala ya usafi, na kujiepusha na viashiria vya rushwa.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Ndg Aron Kagurumjuli, alipokuwa akitoa ufafanuzi wa mada za kikao kazi hicho, ameahidi kutekeleza maelekezo na  maagizo yaliyotolewa na Mkuu huyo wa Wilaya, kwa  kuwataka watendaji wa Kata na mitaa kuwa na takwimu sahihi za maeneo yao zikihusisha taarifa za wakazi, wafanyabiashara, masoko, maeneo ya uvuvi kwa waliopakana na bahari, wafugaji waliopo na aina ya mifugo wanayofuga, pamoja na takwimu sahihi za vibali vya ujenzi.

Pia amewataka watendaji hao kuhakikisha wanazingatia misingi na mkondo wa mawasiliano ulio sawia,  wanajiepusha na migogoro ya kiutendaji, na kuzungukia maeneo yao ya kazi na si kukaa ofisini.

Aidha katika kikao kazi hicho, kilichoshirikisha wataalam kutoka sekta ya afya, biashara, mifugo, uchumi, Utumishi, kilimo, na elimu, kitaendesha mada sita ambazo ni wajibu na majukumu ya watendaji wa Kata, Usimamizi wa uendelezaji wa Miji, Usimamizi na uendelezaji wa daftari la mfanyabiashara, hatua sahihi za uanzishwaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo, pamoja na taratibu za manunuzi.

Hii ni mara ya kwanza kwa Mkuu huyo wa Wilaya kukutana na Watendaji wa Kata na Mitaa wa Manispaa ya Kinondoni tangu kuteuliwa kwake kuitumikia Wilaya hiyo.


Imeandaliwa na

Kitengo cha Uhusiano na Habari.

Manispaa ya Kinondoni.

Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.