• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

MAFUNZO YA WALIMU WAKUU KUHUSIANA NA MTAALA MPYA YAFUNGULIWA RASMI KINONDONI

Tarehe iliyowekwa: May 30th, 2024

Semina ya mafunzo maalum kwa walimu wakuu wa shule za msingi za serikali na binafsi  inayolenga kutoa mafunzo yanayohusiana na utekelezaji wa mtaala mpya wa elimu imefunguliwa rasmi katika Wilaya ya Kinondoni Mei 30 2024 katika ukumbi wa Soko la Magomeni. Mafunzo haya yamepangwa kwa lengo la kuwajengea uwezo walimu wakuu ili waweze kuelewa na kutekeleza mabadiliko ya mtaala kwa ufanisi katika shule zao.

Akizungumza katika Ufunguzi wa Semina hiyo  Mthibiti Mkuu Ubora  wa Shule Manispaa ya Kinondoni ambaye ndiye Mgeni Rasmi katika semina hiyo Bi.Naitwa Solomon Mghumba alitoa shukrani kwa Serikali kutoa mafunzo hayo kwa walimu wakuu na kuahidi kuunga mkono mafunzo hayo kwa kuanzisha na kuendeleza mafunzo ya ziada ya ziada kwa walimu ili waweze  kuelewa na kuendana na mtaala mpya wa elimu.

"Tunashukuru na kuipongeza serikali kwa kutoa mafunzo haya.Kinonfoni tumeyapokea vizuri mafunzo haya na sisi tutaendelea  kuandaa mafunzo yetu ya ndani ili kuwajengea walimu uwezo utakaowasaidia kuwafundisha wanafunzi  vizuri na wataalam bora wa baadaye."

Washiriki wa mafunzo haya ikiwemo  Waratibu wa Mafunzo ngazi ya Mkoa na Wilaya, Wawezeshaji na Walimu Wakuu  walipata fursa ya kujadili na kuelewa vipengele mbalimbali vya mtaala mpya, ikiwa ni pamoja na mbinu za ufundishaji, tathmini za wanafunzi, na matumizi ya teknolojia katika kufundishia. Aidha, walimu wakuu walihimizwa kuwa viongozi na mfano bora katika shule zao, wakihakikisha kuwa mtaala mpya unatekelezwa kikamilifu.

Mafunzo haya yatakayofanyika kwa siku mbili kuanzia Mei 30 2024 mpaka Mei 31 2024 yanatarajiwa kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya Elimu ya Msingi katika Wilaya ya Kinondoni, huku yakitoa mwongozo muhimu kwa walimu wakuu katika kuboresha ufundishaji na ujifunzaji. Serikali na wadau wa elimu wameeleza kuwa wataendelea kutoa msaada na rasilimali zinazohitajika ili kuhakikisha kuwa mtaala mpya unafanikiwa.

Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.