Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Bi.Hanifa Suleiman Hamza, Oktoba 23, 2024 ameongoza kikao cha mafunzo kwa viongozi (Wenyeviti na Makatibu) wa Vyama vya Siasa kutoka Manispaa ya Kinondoni. Mafunzo hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni.
Katika kikao hicho aliwataka viongozi wa vyama hivyo kuzingatia Sheria na Kanuni wakati wa Kampeni za Uchaguzi wa Serikali wa Mitaa itakapowadia ili ziwe za amani na utulivu.
Aidha, Katibu Mkuu Mwandamizi Mkuu Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania, Bi.Edna Stephen Assey, aliwataka viongozi hao kuendesha shughuli zao za kisiasa kwa kuzingatia Kanuni, Sheria na miongozo waliopewa wakati wa usajili wa vyama hivyo na kuepukana na vitendo vya rushwa.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.