• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

"MAANISPAA YA KINONDONI NA SHULE ZAKE NDIO WAMEKUWA WA KWANZA NDANI YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA".

Tarehe iliyowekwa: October 21st, 2017

 NI KAULI YAKE SULEIMAN JAFO WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAISI TAMISEMI KUFUATIA UFAULU WA ASILIMIA 93.3%MATOKEO YA DARASA LA SABA KITAIFA 2017

 Manispaa ya Kinondoni imepongezwa kwa kuongoza katika ufaulu wa asilimia 93.3% wa matokeo ya darasa la Saba Kitaifa kwa mwaka 2017 

 Pongezi hizo zimetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mh Suleiman Jafo alipokuwa akiongea na waalimu pamoja na wazazi wa shule ya Msingi oysterbay hafla iliyofanyika katika ukumbi wa shule hiyo. 

 Amesema kuwa ufaulu huo ni zawadi tosha kwake yeye kama msimamizi wa shule zote katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, na ni kutokana na Juhudi na ushirikiano katika kutekeleza azma ya malengo waliojiwekea 

 "Mimi ninaspecial message kwa shule hii ya Oysterbay lakini kwa Manispaa nzima ya Kinondoni, Naomba nitoe neno langu la Shukrani sana kwamba kwa zawadi kubwa mlionipa kuanzia Jana nikiwa msimamizi wa shule zote katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Manispaa ya Kinondoni na shule zake ndio wamekuwa wa kwanza ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. "Amesema Jafo.

 Naye Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg Aron Kagurumjuli amewapongeza waalimu pamoja na wanafunzi wahitimu wa darasa la saba mwaka huu wa 2017  kwa juhudi kubwa walioifanya kuhakikisha shule za Kinondoni zinafanya vizuri katika ufaulu. 

 Amesema ni kutokana na maarifa, utashi na weledi wa waalimu kwa kufanya kazi kwa  pamoja kwa kushirikiana na uongozi mzima kuhakikisha mwanafunzi anapata kile anachostahili na kwa wakati 

 "Swala la ufaulu wa mtihani wa darasa la saba kwa Manispaa ya Kinondoni imetokana na juhudi zetu za kazi, juhudi binafsi za kazi, na moyo wa waalimu wetu kufanya kazi kujitolea kufundisha mpaka masaa ya ziada ,kutoa mazoezi ya kutosha kwa wanafunzi, ndicho kilichotufanya Manispaa ya Kinondoni kuibuka kidedea " Amebainisha Kagurumjuli. 

 Katika hatua nyingine Afisa Elimu Msingi wa Manispaa hiyo Bw. Kiduma Mageni amezitaja idadi ya shule zilizofanya mtihani wa darasa la Saba kuwa ni shule 135, kati ya hizo za Serikali ni 76, na 59 ni shule za binafsi. 

 Amesema kwa Kinondoni wanafunzi waliofanya mtihani huo jumla yake ni 11,721, na  imepata ufaulu wa asilimia 93.3%, kitakachopelekea wanafunzi wengi kwenda Sekondari. 

 Hongera uongozi mzima, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi, Afisa Elimu, Wakuu wa Shule, pamoja na Menejimenti timu kwa kufanya kazi kwa ushirikiano, na wanafunzi kwa ufaulu mzuri wa matokeo ya darasa la Saba 2017.

 Hii ni kuonyesha uongozi uliotukuka, wa kufanya kazi kwa pamoja na kushirikiana ili kufikia lengo na kutekeleza azma na mikakati mliyojiwekea. 

 Imetolewa na
 Kitengo cha Uhusiano
 Manispaa ya Kinondoni.

Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.