Kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani Disemba 1, 2024, maambukizi ya virusi vya UKIMWI yashuka katika Wilaya ya Kinondoni.
Akitoa taarifa ya hali ya Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI katika Maadhimisho ambayo yamefanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers Kiwilaya leo Novemba 29, 2024, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dkt. Peter Nsanya, amesema kuwa, Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI Wilaya ya Kinondoni yameshuka kutoka 4.7% Mwaka 2023 mpaka 4.2% Mwaka 2024.
Aidha, Dkt Nsanya amesema kuwa juhudi za dhati ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Wilaya ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali zimesaidia pakubwa katika mafanikio hayo.
"Hapa tulipofikia bado tunaendelea na mapambano zaidi kama kauli mbiu ya Mwaka huu isemayo, "Chagua njia sahihi, Tokomeza UKIMWI" amesema Dkt Nsanya.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.