Imeelezwa kuwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika Mkoa wa Dar es Salaam yamepungua Kwa asilimia 0.2
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Albert Chalamila, alieleza hayo Desemba Mosi, 2024 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Viwanja vya Zakheem, Wilayani Temeke.
Mheshimiwa Chalamila alisema kuwa, "maambukizi yamepungua kutoka asilimia 4.7 hadi 4.5. Nawapongeza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Hamashauri zote kwa kueendele kupinga maambukizi haya."
Katika kuendelea na jitihada za kupinga maambukizi mapya, Mheshimiwa Chalamila aliwataka Wakurugenzi kuendelea kutenga bajeti kutoka Mapato ya ndani, Mikopo ya asilimia Kumi kuwagusa Waviu, na kuboresha Sheria mdogo za Halmashauri ili kukabiliana na janga hilo.
Aidha Mhe. Chalamila aliwataka Wauguzi kuzingatia malengo ya Kitaifa katika kudhibiti UKIMWI na kutoa elimu katika jamii na jinsi ya kujikinga dhidi ya maambukizi hayo.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.