• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

KINONDONI YATOA TUZO KWA WAALIMU NA SHULE ZILIZOFANYA VIZURI UFAULU WA MATOKEO YA DARASA LA SABA KWA MWAKA 2017

Tarehe iliyowekwa: November 16th, 2017

 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni leo imetoa tuzo, vyeti pamoja na fedha taslimu kwa wakuu wa shule, waalimu wa masomo pamoja na Kata zilizofanya vizuri katika ufaulu wa matokeo ya mtihani wa darasa la saba kwa mwaka 2017.

 Tuzo hizo zimetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Alli Hapi alipokuwa mgeni rasmi katika tafrija za kuwapongeza waalimu hao zilizofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi mbuyuni. 

 Amesema tuzo hizi ni kutokana na matokeo mazuri ya ufaulu kwa mwaka huu ambapo yameiweka Kinondoni katika kilele cha Taifa na hii ni kuonyesha ushirikiano, juhudi, maarifa na weledi wa waalimu wetu pamoja na viongozi wetu. 

 "Matokeo ya mwaka huu yametuweka katika kilele chá Taifa, rekodi hii iliyotokea mwaka huu, ama haijawahi kutokea kabisa , tumevunja rekodi katika historia ya Wilaya na Manispaa ya Kinondoni, Jambo hili sio Jambo la kubeza kwa sababu linatasfiri juhudi, ushirikiano na kazi kubwa ambayo viongozi wetu wameifanya. "Amesema Hapi 

 Naye Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mh Benjamin sitta amesema lengo ni kutaka watanzania waelewe umuhimu na faida ya Elimu bure iliyosaidia kupunguza utoro, hali iliyopelekea wanafunzi wote kuhudhuria vipindi na kufanya mitihani kwa umakini. 

 Ameongeza kuwa lengo pia ni kuwapa moyo na kuthamini kazi nzuri na mchango wao mkubwa walioufanya katika kuhakikisha Kinondoni inaibuka kidedea katika ufaulu wa matokeo ya mtihani wa darasa la saba kwa mwaka 2017.

 Naye Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg Aron Kagurumjuli ameainisha makundi yaliyopata tuzo hizo pamoja na zawadi kuwa ni walimu wakuu wa shule 78, zenye ufaulu zaidi,  shule 10 zenye mabadiliko makubwa zaidi katika ufaulu, waalimu waliofundisha kikamilifu na kwa weledi na kutoa  "A" nyingi kwenye masomo yao pamoja na kata zilizofanya vizuri. 

 Ameongeza kuwa Kinondoni imedhamiria na imejipanga kuelekea 2018, inashikilia rekodi hii kwa kufanya kazi kwa umakini na weledi  mkubwa kwani ndiyo nguzo na silaha ya mafanikio. 

 Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Alli Hapi amewataka waalimu kuhakikisha wanaendeleza juhudi hizo ili kufikia malengo mazuri na makubwa katika sekta ya elimu kwani ndio ufunguo wa maisha. 

 Tafrija hii imehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Baraza la madiwani, wenyeviti wa Serikali za Mitaa, wawakilishi kutoka Bank ya NMB pamoja na wakuu wa idara na vitengo wa Manispaa ya Kinondoni. 

 Imetolewa na
 Kitengo cha Uhusiano na Habari
 Manispaa ya Kinondoni

Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.