• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

KINONDONI YASAINI MKATABA WA LISHE, KWA LENGO LA KUTEKELEZA SERA YA LISHE KWA VITENDO

Tarehe iliyowekwa: November 9th, 2018

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, katika utekelezaji wa sera na maelekezo ya Wizara  ya Afya maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto na OR-TAMISEMI imesaini mkataba wa lishe utakaotumika kutekeleza mapango jumuishi wa lishe wa Kitaifa(NMNAP) wa mwaka 2016-2017/2021, kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Akisaini mkataba huo kati yake na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Daniel Chongolo,  Mkurugenzi wa Manispaa hiyo  Ndg Aron Kagurumjuli amesema Manispaa yake iko tayari na imejipanga vizuri kuanza ukurasa mpya wa utekelezaji wa afua za lishe kwa ufanisi na kwa vitendo,  na kwa kuzingatia mahitaji ya mkataba huo, kwani kwa kufanya hivyo itakua imeenda sambamba na uboreshaji wa afya ya mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano,  kwa kumpatia lishe bora na yenye afya kwa mujibu wa  miongozo, sera, na kanuni katika kufikisha tija inayokusudiwa.

Akifafanua mahitaji yaliyoko katika sera hiyo ya lishe,  Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Dkt. Festo Dugange amesema Sera hiyo inasisitiza kila Halmashauri kutenga bajeti ya kiasi cha tsh 1000/=kwa kila mtoto wa umri chini ya miaka 5, kutoka mapato ya ndani, kwa lengo la kutekeleza shughuli za lishe kwenye maeneo ya kipaumbele.

Ameyataja maeneo hayo ya kipaumbele kuwa ni  watoto kupata vyakula vyenye virutubisho sahihi na kwa kiasi kinachostahili, kuhakikisha elimu ya lishe inatolewa kikamilifu kwa wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano, kuhakikisha watoto wenye utapiamlo mkali wanapatiwa matibabu stahiki, na kufanya kaguzi za vyakula hasa chumvi zenye madini  joto.

Nyingine ni kuhakikisha wajawazito wanapatiwa madini chuma na vidonge vya Foliki Acid ili kuzuia upungufu wa damu na matatizo yanayosababishwa na ukosefu wa madini hayo kwa watoto, kutekeleza vikao vya Halmashauri vya kamati ya lishe kila robo kwa lengo la kufanya tathmini ya hali ya lishe na kuhakikisha wanashirikiana na wadau mbalimbali wa lishe walioko katika Halmashauri kwa lengo la kufanikisha.

Hafla hiyo ya kutiliana saini mkataba huo iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya,  imehudhuriwa pia na Katibu tawala wa Wilaya hiyo Bi. Stella Msofe, na Afisa lishe wa Manispaa hiyo Bi. Emiliana Sumaye

Imeandaliwa na

Kitengo cha Uhusiano na Habari.

Manispaa ya Kinondoni.

Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.