• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

KINONDONI YAPOKEA MIFUKO 400 YA CEMENTI KUTOKA KANISA LA INUKA UANGAZE

Tarehe iliyowekwa: January 25th, 2019

Akipokea mifuko hiyo ya cementi kutoka kanisa la Inuka uangaze linaloongozwa na Mtume Boniface Mwamposa,  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Daniel Chongolo amesema imekuja wakati muafaka kwani  itasaidia kuleta hamasa ya nguvu ya wananchi katika kuhakikisha kunakuwepo na mafanikio ya utatuzi wa  changamoto kubwa ya  madarasa iliyoko Wilayani hapo.

Amesema Serikali ya awamu ya tano dhamira yake kuu ni kuboresha miundombinu ya elimu pamoja na mfumo wake, hivyo mifuko hiyo  imekuja kipindi ambacho Wilaya yake imepanga kufikia mwezi wa tatu mwaka huu iwe imekamilisha madarasa mia moja.

"Tunamshukuru na kumpongeza Mchungaji na Mtume Mwamposa pamoja na kanisa lake lote, kuona umuhimu wa kuchangia swala la elimu, niseme tu kwamba Msaada huu wa mifuko ya cement umekuja wakati mwafaka, kwani  tulishajiwekea malengo mkakati ya kutatua changamoto iliyopo mbele yetu ya vyumba vya madarasa kwa kushirikiana na nguvu za wananchi kuhakikisha  tunajenga mdarasa mia moja ifikapo mwezi wa tatu, ikiwa ni hatua za awali za  kuhakikisha tunakabiliana na  upungufu wa vyumba vya madarasa katika Wilaya yetu.".Amebainisha Chongolo

Ameongeza kuwa Jamii yetu inajengwa na taasisi mbalimbali ambazo kwa pamoja zikishirikiana na serikali zitaleta Matokeo chanya, hivyo tukio la leo limedhihirisha nia thabiti mliyonayo ya kumuunga mkono Mh. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ya kuboresha miundombinu ya elimu Nchini.

Akikabidhi mifuko hiyo, Mchungaji na Mtume Boniface Mwamposa amesema ni katika kuunga mkono juhudi za Mh Rais katika kuboresha sekta ya Elimu, kadhalika ni kutekeleza agizo la Mungu, kwani hata biblia imeandika katika kitabu cha  Mithali 4:13 kuwa "mkamate sana elimu, usimwache aende zake mshike, maana yeye ndo uzima wako" na kuahidi kuendelea kusaidia swala zima  la elimu pale inapopasa.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe Benjamin Sitta katika kushuhudia ugawaji huo wa mifuko ya cement ameupongeza uongozi mzima wa kanisa hilo kwa azma njema waliyonayo katika elimu, na kuzihamasisha taasisi nyingine kufanya hivyo ili kuleta tija katika sekta hii Muhimu ya Elimu katika Taifa letu.

Imeandaliwa na

Kitengo Cha Habari na Uhusiano

Manispaa ya Kinondoni.

Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.