• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

KINONDONI YAADHIMISHA SIKU YA WATU WENYE ULEMAVU DUNIANI KWA VITENDO

Tarehe iliyowekwa: December 3rd, 2020

Kinondoni kwa kushirikiana na  shirika la Engender Health Imeadhimisha siku ya watu wenye ulemavu duniani yenye kauli mbiu isemayo "Si kila ulemavu unaonekana", kwa kutoa huduma  za afya ya uzazi bure kwa kundi la watu wenye ulemavu.

Maadhimisho hayo  yamefanyika katika kituo kipya cha  Afya cha Kigogo ambapo watu wenye ulemavu wamepata huduma mbalimbali za afya ya uzazi ikiwa ni pamoja na upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi, Ushauri juu ya matumizi ya uzazi wa mpango, masuala ya ukatili wa kijinsia pamoja na huduma nyingine za kiafya.

Akiongea wakati wa maadhimisho hayo, Mratibu wa ubora wa huduma za afya toka Kinondoni, Dkt Zuhura Manyama amesema wameadhimisha siku hii katika kituo cha afya ili kufikisha ujumbe kwa Jamii kuwa walemavu pia wanayo haki ya huduma za afya ya uzazi kama watu wengine na kuwataka wauguzi wa afya kusimamia misingi yao ya kazi inayowataka kutoa huduma sawa kwa wote na si vinginevyo.

"Wenzetu ambao wana ulemavu waelewe kwamba Wana haki sawa na raia wengine wote, wao Kama wananchi wanapata huduma hapa wanastahili kupewa huduma sawasawa na wale wengine, huduma ambazo Zina ubora uleule" Amesisitiza Dkt Zuhura

Naye Mkurugenzi wa Shirika la  Engender Health Bi Prudence Masako amesema shirika lake linashirikiana na  Serikali katika kutoa huduma bora za Afya kwa watu wote, hivyo kwa leo wameamua kusaidia huduma za afya kwa kundi la watu wenye ulemavu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku yao muhimu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa mradi wa scalling of family planning programs wa Engender Health Dkt  Moke Magoma amesema kuwa wenzetu wenye ulemavu ni sehemu ya kipaumbele cha Mradi, hivyo shirika limefarijika kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni kupitia kamati ya uendeshaji wa afya ya Halmashauri kwa kuwapa huduma watu wenye ulemavu.

Katika hatua nyingine Mratibu wa Umoja wa wanawake viziwi Tanzania ( UWAVITA) Bi Aneth Mdemu ameishukuru Manispaa ya Kinondoni kwa niaba ya wenzie wanaoishi na ulemavu kwa kuwasogezea huduma za afya ya uzazi karibu  na jamii yao na pia kwa kupata elimu ya masuala mbalimbali yanayohusu Afya  kupitia wakalimani wa lugha ya alama.

Siku ya watu wenye ulemavu Duniani huadhimishwa kila tarehe 3 mwezi Disemba ambapo , kwa mwaka huu kitaifa yanaadhimishwa Mkoani Dodoma.

Imeandaliwa na

Kitengo cha Habari na Uhusiano

Manispaa ya Kinondoni

Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.