• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

KAMPENI YA KUGAWA DAWA ZA MINYOO, MATENDE NA MABUSHA YAZINDULIWA KINONDONI

Tarehe iliyowekwa: November 21st, 2022

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni Bi.  Stella Msofe leo Jumatatu, Novemba 21, amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Mhe. Amos Makalla katika  uzinduzi wa zoezi la utoaji wa dawa za minyoo, matende na mabusha kimkoa  lililofanyika katika shule ya msingi Tandale, Kata ya Tandale Wilaya ya Kinondoni.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, aliwataka wananchi wote wa mkoa wa Dar es Salaam   kushiriki kikamilifu ili kufikia lengo la kuwezesha walengwa wote wenye umri wa miaka mitano na kuendelea kupata dawa za kudhibiti madhara ya magonjwa hayo kwa kushirikiana na watoa huduma na viongozi wa Serikali za mitaa kama yalivyofanikishwa mazoezi mengine zikiwemo chanjo mbalimbali zilizofanyika kwa nyakati tofauti kwa mafanikio.

Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuondokana na fikra na dhana  potofu zinazoenezwa na Watu wasio na nia njema kuwa dawa hizo zina madhara kwani hazina ukweli na zimethibitishwa kitaalamu kuwa ni salama.

Alisisitiza kuwa hakuna Serikali ambayo inawapenda watu wake kama ya Tanzania inayoweza kuwaletea wananchi wake kitu chenye madhara badala yake inapambana kuwaletea tiba kinga ya kupunguza au kuondoa madhara ya magonjwa haya hususani katika Wilaya za Kinondoni na Temeke zilizothibitika kuwa na maambukizi makubwa katika mkoa wa Dar es Salaam.

Katika uzinduzi huo wataalam wa Afya walianza kwa kutoa maelezo  ya vigezo vya ugawaji wa dawa hizo kwa kuzingatia umri, kimo na uzito kisha kutoa dawa kwa kuzingatia vigezo hivyo.

Waliohudhuria katika uzinduzi huo na kunywa dawa hizo ni pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni Bi. Stella  Msofe ambaye alikuwa mgeni rasmi, mwakilishi wa  Wizara  ya Afya kutoka Makao Makuu Dodoma, mwakilishi kutoka TAMISEMI, Mganga Mkuu wa Mkoa, Mganga Mkuu wa Wilaya, wawakilishi wa dini, Walimu, wanafunzi , Wakazi wa Tandale na Wadau wengine wa Afya katika Mkoa wa Dar es Salaam wakiwemo wawakilishi  kutoka MDH.

Wakizungumza katika ugawaji wa dawa hizo za kinga Tiba wote walisisitiza kuwa kuwa dawa hizo zimethibitishwa kitaalam kuwa ni salama na hazina madhara na kwamba wasioruhusiwa kutumia ni watoto chini ya umri wa miaka mitano na wajawazito.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini:

HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI.

Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.