• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

HALMASHAURI ZOTE NCHINI ZATAKIWA KUSALIMISHA WATANZANIA KWA KUSHIRIKI OPERESHENI MAALUM IENDAYO KWA JINA LA "TUDHIBITI UCHAFUZI WA MAZINGIRA TUSALIMIKE ".

Tarehe iliyowekwa: November 1st, 2017

 NI AGIZO LAKE NAIBU WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS MAZINGIRA MH. KANGI LUGOLA KUFUATIA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIA NCHI ZINAZOSABABISHWA NA NCHI ZILIZOENDELEA KUCHAFUA ANGA HEWA. 

 Halmashauri zote nchini zimetakiwa kuhakikisha zinasalimisha  watanzania kwa kushiriki operesheni maalumu ya kusafisha mitaro na kuondoa takataka kwenye kingo za mito  iitwayo "TUDHIBITI UCHAFUZI WA MAZINGIRA TUSALIMIKE " inayotarajia kuanza tarehe 01/11/2017, ili waweze kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

 Agizo hilo limetolewa leo na Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mh Kangi Lugola alipokuwa katika ziara yake kutembelea maeneo yaliyoathirika na mvua  ambapo leo alikuwa Tandale kwa Mtogole. 

 Amesema kampeni hiyo itadumu kwa muda wa miezi miwili na itazinduliwa kwa kufanya usafi kwenye kingo za mito, madaraja na pembezoni mwa barabara ili tuweze kukabiliana na athari hizi zinazopelekea maji kuongezeka na kuathiri kingo za bahari. 

 "Tanzania yetu hii tunayoifahamu kwa muda sasa tumeanza kukumbwa na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi, athari hizi zinasababishwa na nchi zilizoendelea wanavyochafua anga hewa, na matokeo yake sasa tunaanza kupata athari hizi "Amesema Naibu Waziri 

 Ameongeza kuwa uzinduzi huo utafanyika eneo la mtogole Kwa kuwa ni eneo ambalo linakumbwa na athari za mafuriko, kutokana na uchafu wa Mazingira pamoja na miundombinu ya barabara na mito kutokuwa rafiki.

 "Sasa juzi ile mafuriko mliyoyaona ambayo yamesababisha baadhi ya miundombinu, mabarabara madaraja kuharibika makazi ya watu kuingia mafuriko, kupoteza maisha ya watu  pamoja na mali zenu ,ndilo chimbuko la kuanzisha operesheni hii "Amesisitiza Naibu Waziri. 

 Ameongeza kuwa ni chimbuko kutokana na kuwepo kwa mrundikano wa taka ngumu kama vile plastic, matambara na chupa za maji ambazo kwa asilimia tisini zimezalishwa na wanadamu.

 Naye Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Ndg Joseph Malongo ameahidi kutekeleza agizo hilo la Naibu Waziri kwa kuwapatia wakurugenzi wa Halmashauri zote waraka utakaotoa mwongozo na maelekezo ya utekelezaji wa agizo la operesheni hiyo .

 Kwa nyakati tofauti Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Ndg Aron Kagurumjuli alipotakiwa kuzungumnzia changamoto za kutozolewa takataka kwa wakati kwenye Halmashauri yake amesema Manispaa inao utaratibu wa kuzoa taka kwenye maeneo ya Umma kama vile kwenye masoko, na kwenye mitaa wanao utaratibu unaoeleweka kabisa wa kuchangisha fedha kwa utaratibu na zinapotimia kutafuta mkandarasi wa kuzoa taka kwa kumsimamia wenyewe. 

 "Kila mtaa unapaswa kukodi mkandarasi atakayebeba takataka kutoka kwenye mtaa wake, kutokana na fedha walizochangisha, kwa hiyo sio Manispaa kuja kuzoa taka hapana, wao wenyewe kwenye Mitaa wanachangishana fedha kwa mujibu wa utaratibu, hii inafanyika Manispaa nzima lakini pia Manispaa kama Manispaa inawajibika kwenda kuzoa takataka kwenye maeneo ya Umma kama masoko "Amefafanua Kagurumjuli. 

 Katika hatua nyingine Naibu Waziri amewataka wananchi kuwa na tabia ya kuzikusanya taka na kuzitupa kwenye maeneo sahihi kama madampo na sio kuzitupa kwenye kingo za mifereji, mitaro ya maji pamoja na pembezoni mwa barabara. 

 Operesheni hii Maalum yenye kauli mbiu isemayo   "Tudhibiti uchafuzi wa Mazingira tusalimike "itadumu kwa miezi miwili kuanzia tarehe 01/11/2017

 Imetolewa na
 Kitengo cha  Habari na Uhusiano
 Manispaa ya Kinondoni.

Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.