• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

DC CHONGOLO AWAONYA WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI KINONDONI

Tarehe iliyowekwa: January 17th, 2020

NI KUHUSIANA NA TARATIBU ZA KUWAPOKEA WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amewaagiza wakuu wa shule zote za Sekondari katika Wilaya hiyo kuacha mara moja tabia ya kuwazuia wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza kuanza masomo kutokana na kutokamilisha mahitaji yao ya shule.

 Ametoa agizo hilo jana wakati wa sherehe za kuwapongeza walimu kwa ufaulu mzuri wa mitihani ya kumaliza elimu ya msingi  kwa mwaka 2019 ambapo Kinondoni imepata ufaulu wa asilimia 97.17 na kuwa ya  tatu kati ya Halmashauri 186 kitaifa, hafla iliyofanyika ukumbi wa officers Mess

Amesema kuwa zipo baadhi ya shule ambazo zinawazuia wanafunzi kujiunga na masomo kwa kile wanachokidai kutokamilisha mahitaji ya shule na kuzitaka shule za Kinondoni kutojihusisha na tabia hiyo bali kuwa sehemu ya  kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano inayotekeleza sera  madhubuti  ya elimu bila malipo inayoenda sambamba na uchumi wa viwanda.

“Kuna baadhi ya maeneo nimesikia kuna wakuu wa shule wanawarudisha nyumbani watoto kwa sababu hawajakamilisha mahitaji yao, kama mtoto hana viatu, sijui nini waache wasome wakati wazazi wao wanawatafutia mahitaji hayo, naomba nisi sikie mwanafunzi amerudishwa nyumbani kwenye wilaya yangu” amesisitiza Mhe. Chongolo.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Benjamini sitta amesema kuwa mafanikio ya kufanya vizuri kwa wanafunzi wa darasa la saba mwaka 2019 kwenye Halmashauri hiyo ni uthibitisho tosha unao onesha namna walimu, wazazi na wanafunzi wanavyoshirikiana kikamilifu katika nyanja ya elimu na hivyo kutoa wito kwa wazazi kuendeleza ushirikiano huo katika usimamizi wa wanafunzi hususani kwenye masuala ya taaluma.

Kaimu Afisa elimu wa Halmashauri hiyo, Bi Chitegets Dominick pia alifafanua jumla ya wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani huo walikuwa 12,619, wavulana 6,115 na wasichana 6,450, huku walioganya wakiwa 12,523, wavulana 6,058 na wasichana 6,465.

Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ndugu Aron Kagurumjuli kwa usimamizi mzuri wa elimu na kwamba anatambua jitihada zake za kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanapata elimu bila malipo na kwamba anatimiza kimamilifu majukumu na maagizo yanayotolewa na Rais Dk. John Magufuli

Imeandaliwa na

Kitengo cha na Habari na Uhusiano

Manispaa ya Kinondoni.

Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.