• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fukwe na Visiwa
    • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Matukio ya Utalii
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Meya
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Iliyopangwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Habari

DC CHONGOLO AWAFUNDA VIJANA WAJASIRIAMALI WA BIDHAA ZA NGOZI KUCHANGAMKIA FURSA ZA MIKOPO YA HALMASHAURI

Tarehe iliyowekwa: November 14th, 2019

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amewataka vijana kutumia fursa inayotolewa na serikali kupitia halmashauri kupata mikopo isiyokuwa na riba ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Mhe. Chongolo alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua mafunzo kwa vijana wajasiriamali wanaotengeneza bidhaa za ngozi waliopo katika Manispaa ya Kinondoni ambapo miongoni mwao walipata fursa ya kushiriki maonesho ya wakulima nanenane.

Mhe. Chongolo alisema kuwa Manispaa ya Kinondoni inafungu la bajeti kwa ajili ya kutoa mikopo kwa Vijana, wakina mama na watu wenye ulemavu kwa lengo la kuwasaidia kujikwamua katika umasikini hivyo vijana wanapaswa kutumia nafasi hizo wanazozipata kwani itawawezesha kukuza mitaji yao na hivyo kufikia lengo la kuwa na viwanda huku akitolea mfano wa mfanyabiashara mkubwa Marehemu Dk. Reginal Mengi ambaye alifanikiwa kuwa na viwanda kupitia ujasiriamali.

Alifafanua kuwa iwapo watatumia vizuri mafunzo hayo yataleta tija katika kukuza uchumi wa ndani na kwamba serikali kupitia halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni itasimamia kupata mikopo hiyo na hivyo kuwawezesha kupata mashine pamoja na eneo la kujenga kiwanda chakutengeneza bidhaa za ngozi.

“ Nawapongeza sana idara husika ambayo imeandaa haya mafunzo sambamba na maonyesho ya bidhaa za ngozi, vijana mliopo hapa ,tumieni hii fursa mliyoipata, hakuna mafanikio ya siku moja, wote waliofanikiwa walianza kama nyie hapa” alisema Mhe. Chongolo.

“ Tunahitaji watu ambao watakuwa na nia ya kweli ya kujikwamua kiuchumi, inawezekana kuzalisha bidhaa za ngozi kwakuwa Tanzania tunaongoza kwakuwa na mifugo, ukiangalia Dar es Salaam ndio inaongoza kwa kula nyama,kwahiyo tunazana za kutengenezea bidhaa zetu” alifafanua.

Kwaupande wake , Meneja ukuzaji Bidhaa kutoka Tan Tredi , Masha Husein alisema kuwa wataendelea kushirikiana na manispaa ya Kinondoni katika kuwaelimisha wajasiriamali namna ya kufanya biashara kwenye maonesho kwani hiyo imekuwa ni changamoto kubwa kwao.

Alifafanua kuwa, wajasiriamali wengi hawana uelewa wa kutosha kuhusiana na namna ya kushiriki kwenye maonesho mbalimbali wanapopata nafasi jambo ambalo kama Tan Tredi imeliona na hivyo kusisitiza kuwa watahakikisha wanatoa elimu hiyo ili waweze kunufaika.

Naye Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Dk. Patricia Henjewele alimpongeza Mhe. Chongolo kwakujali vijana na kusema kuwa katika maonesho ya nane nane waliona umuhimu wakukutana na wajasiriamali hao na hivyo kuandaa semina hiyo iliyoambatana na maonesho.

Aidha aliwapongeza Tan Tredi kwakuwezesha maonesho hayo na hivyo kuahidi kuendeleza ushirikiano zaidi katika kutoa elimu kwa wajasiriamali hao.


Imetolewa na

Kitengo cha Habari na Uhusiano

Manispaa ya Kinondoni.

Matangazo

  • PONGEZI June 07, 2023
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI-DEREVA DARAJA II April 24, 2023
  • MABADILIKO YA SIKU YA MAFUNZO YA WASIMAMIZI WA MAUDHUI, WASIMAMIZI WA TEHAMA NA MAKARANI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 July 28, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • AFISA ELIMU MSINGI KINONDONI APONGEZWA

    May 19, 2023
  • JAPAN YAIPATIA MSAADA MZIMUNI SEKONDARI

    March 15, 2023
  • VIKUNDI VYAASWA MATUMIZI SAHIHI YA MIKOPO

    February 18, 2023
  • "HAKUNA TIMU KUBWA ZAIDI YA KMC FC"

    February 18, 2023
  • Tazama zote

Picha Jongefu

VITUO VITANO VYA MSAADA WA MFUMO WA TAUSI, KITUO CHA MIITO YA SIMU KUBORESHA UKUSANYAJI WA MAPATO
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • TARATIBU ZA KUPATA KIBALI CHA UJENZI
  • TAARIFA KWA UMMA
  • RATIBA YA MSTAHIKI MEYA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255 22 2170173

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.