• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

DC CHONGOLO AAGIZA WATA ALAMU WA AFYA KUTOA ELIMU YA KUJIKINGA NA CORONA KWA WANANCHI

Tarehe iliyowekwa: March 19th, 2020

NI KATIKA VITUO VYA DALADALA, NYUMBA ZAIBADA

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo, amewaagiza wata alaamu wa Afya Wilayani hapo kuanza mara moja kutoa elimu ya kujikinga na virusi vya Corona kwenye nyumba za Ibada ikiwemo Makanisani na Misikitini.

Aidha Mhe. Chongolo ameagiza pia elimu hiyo kutolewa kwenye vituo vya daladala ili kuwasaidia wananchi kutambua namna ya kutumia na kujikinga na Virusi hivyo.

Mhe. Chongolo ametoa agizo hilo leo katika kikao cha zarura kilichofanyika katika ukumbi wa Afya ambapo kimehusisha Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Idara ya Afya, watendaji pamoja na viongozi wa Dini .

Amesema kuwa lengo la kikao hicho cha zarura ilikuwa ni  kujadili namna na hatua zitakazo chukuliwa katika kudhibiti virusi hivyo ili visiweze kusambaa pamoja na kutoa elimu ya kutosha kwa watumishi sambamba wananchi katika Wilaya hiyo.

Amesema kutokana na kuingia kwa Virusi hivyo vya Corona  katika jiji la Dar es Salaam, wataalamu hao wa Afya wa Wilaya hiyo wanapaswa kutoa elimu madhubuti kwenye maeneo ambayo ni lazima wananchi kuyatumia kama vile Vituo vya daladala ikiwemo vya mwendokasi, nyumba zaibada kuhusu namna ya kujikinga na virusi hivyo.

Amefafanua kuwa katika elimu hiyo pia itajikita katika kuelimisha wananchi namna ya kutumia vifaa vya kujikinga na maambukizi hayo kama vile vifaa vya kusafishia mikono, Gloves na Barakoa (Mask ) za kufunika pua na mdomo.

“ Hili jambo tunapaswa kulichukulia kwa tahadhari kubwa, muwaelimishe wananchi kuhusu namna ya kujikinga na Virusi hivyo, pamoja na kutumia hivyo vifaa ,mnapopita kwenye hayo maeneo hakikisheni kwamba mnawaelimisha vizuri ili wajue ni wakati gani wanapaswa kuvitumia, pia kusafisha miko mara kwa mara” amesema Mhe. Chongolo.

“ Lakini pia tuwasaidie wananchi kutoka kwenye presha waliyo kuwa nayo hivi sasa, tunafahamu kuwa watanzania wengi wamepata taharuki juu ya Vizuri hivi, tusipojitahidi tutajikuta tatizo la presha lina adhiri wananchi kuliko Vizuri vya Corona.

Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo amewaeleza viongozi wadini kwamba mikusanyiko isiyokuwa ya lazima haipaswi kuwepo ila kwa ambao wanataka kufunga ndoa wafungishwe lakini kwa kufuata utaratibu ambao utaepusha mikusanyiko ya watu.

Awali Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo, John Kijumbe amesema kuwa hadi sasa wameshachukua tahadhari na kama vile  kutoa elimu katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwa watumishi na wahudumu wa Afya pamoja na kugawa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo.

Hata hivyo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imejidhatiti kikamilifu katika kujikinga na virusi hivyo kwakuweka visafisha mikono kwenye mageti yote ya kuingia ikiwa ni katika kuhakikisha kuwa kila mwananchi anayefika kupata huduma mbalimbali wanakuwa salama.

Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.