• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAMPONGEZA MKURUGENZI KWA UFAULU MZURI WA DARASA LA SABA 2019

Tarehe iliyowekwa: November 28th, 2019

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni  limempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo , Aron Kagurumjuli kwa jitihada zake zakuwezesha kufanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba.

Wakizungumza katika kikao cha robo ya kwanza ya mwaka  kilichofanyika leo, madiwani hao wameeleza kuwa Mkurugenzi Kagurumjuli amekuwa na ushirikiano mzuri na watendaji wake na hivyo kufanikisha kufanya vizuri kwenye matokeo ya darasa la saba.

Naibu Meya wa Halmashauri hiyo, Mhe. George Manyama amesema kuwa kama halmashauri imejipanga kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliomaliza darasa la saba wanapata nafasi ya kusoma na kwamba hakuna atakaye kaa nyumbani.

Amefafanua kuwa ushindi huo uliopatikana ni dira inayoonyesha kuwa hata matokeo ya kidato cha nne yatakuwa mazuri na kwamba Halmashauri ya Kinondoni itaongoza.

“ Niseme tu haya ni matokeo mazuri kwetu, baraza limepitisha maadhimio ya kubadili shule ya msingi Kijitonyama kuwa Sekondari, huu ni mpango uliofanywa na wataalamu wa  Halmashauri yetu, lakini pia bado tunaendelea kufanya upembuzi yakinifu kuangalia shule nyingine ambazo tunaweza kuzigeuza kuwa Sekondari.

Diwani wa Kata ya Mwananyamala  Mhe.Songoro Mnyonge amesema kuwa Halmashauri ya Kinondoni katika matokeo yake ya darasa la saba mwaka huu imeshika nafasi ya tatu kitaifa huku kimkoa ikishika nafasi ya kwanza na kuongeza kuwa matokeo hayo yanatokana na jitihada za Mkurugenzi Kagurumjuli kwani amekuwa akiwasimamia vyema watendaji wake sambamba na kutoa ushirikiano jambo ambalo limewezesha kupata matokeo hayo mazuri.

Amesema kuwa kama madiwani watashirikiana kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliofaulu wanapata nafasi ya kuingia kidato cha kwanza kwakuwa shule zipo na kwamba hakuna mwanafunzi ambaye atakaa nyumbani kwakukosa nafasi.

“ Pamoja na pongezi hizi, ni wakati sasa wakuhakikisha kuwa wote wanakwenda kusoma , kama baraza leo hii tumeadhimia kuwa shule ya msingi Kijitonyama itabadilishwa na kuwa Sekondari, shule hii inavyumba 20 vya madarasa , hivyo wote watapata nafasi ya kusoma” amefafanua Mhe.Songolo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kunduchi Michale Urio , amesema kuwa suala la elimu bure lililotolewa na Mhe. Rais Dk. John Magufuli, limewezesha kuwa na idadi kubwa ya watoto wanaosoma, hivyo Halmashauri itaendelea kuweka jitihada za kuhakikisha kuwa wanapata nafasi za kusoma.


Imetolewa na

 Kitengo cha Habari na Uhusiano

Manispaa ya Kinondoni

Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.