• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Mahesabu
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
      • Bunju
      • Hananasif
      • Kawe
      • Kigogo
      • Kijitonyama
      • Kinondoni
      • Kunduchi
      • Mabwepande
      • Magomeni
      • Makongo
      • Makumbusho
      • Mbezi Juu
      • Mbweni
      • Mikocheni
      • Msasani
      • Mwananyamala
      • Mzimuni
      • Ndugumbi
      • Tandale
      • Wazo
    • Muundo wa Taasisi
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
      • Fukwe na Visiwa
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
    • Utalii
      • Matukio ya Utalii
      • Royal Tour Bus
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
    • Vibali vya Ujenzi Vilivyotolewa
    • Nyaraka za Elimu

BARAZA LA BIASHARA KINONDONI LAZINDULIWA

Tarehe iliyowekwa: December 1st, 2020

Akizindua Baraza hilo, Mwenyekiti wake ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amesema hili ni jukwaa pekee linatoa nafasi ya  kukutana na wadau wa sekta binafsi na  kujadiliana fursa zakiuchumi ikiwa ni pamoja  na utatuzi wa changamoto utakaoleta tija katika mustakabali wa nchi yetu inayosimamia sera ya  uchumi wa kati wa viwanda.

Ameongeza kuwa ni chombo kinachoweza kupaza sauti juu ya masuala yahusuyo sekta binafsi na wafanyabiashara kwa minajili ya maboresho yaliyokuwa makwazo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Amesema "Ni fursa Muhimu Kama wadau kwakuwa wote tunajenga  nyumba moja, tunajenga mustakabali was Nchi yetu, tutakayoyaongea yakajenge Nchi yetu, Tumepata fursa Kama hii tunakwenda kutatua kero zote" Daniel Chongolo.

Akiainisha majukumu ya  kamati za baraza hilo la biashara katibu wake kwa niaba ya Mkurugenzi   ambaye pia ni  Mweka hazina wa Manispaa Ndg Maximilian Tabonwa amesema uundwaji wa Baraza hili ni sehemu ya  majadiliano kati ya sekta binafsi na sekta ya Umma katika ngazi yaTaifa, Mkoa na Wilaya na kuainisha majukumu hayo kuwa ni kufanya tathmini, kuainisha njia ya utekelezaji wa maboresho, kupendekeza utaratibu wa mfumo, kujadili mahitaji ya rasilimali, kujadili ajenda za mikutano na kufuatilia maombi ya kamati tendaji.

Akijibu changamoto iliyoainishwa na wadau kuhusiana na Tax clearance katika kuhuisha leseni za Biashara, Afisa Biashara wa Manispaa hiyo Ndg.Pastori Magodi amesema ni kwa  mujibu wa vifungu vya Sheria vinavyomtaka mfanyabiashara au mtu  yeyote anayehuisha leseni kulazimika kushirikiana na TRA, ili kupata taarifa za awali kuhusiana na leseni hiyo kwa maana ya  kujua kama anadeni la nyuma au la.

Naye Meneja TRA Mkoa wa Kinondoni Ndg Masawa Masatu alipokuwa akifafanua hoja iliyoelekezwa kwakwe kuhusiana na masuala ya ulipwaji wa kodi, amewataka wafanyabiashara kuwa makini na vishoka na kuhakikisha wanafuata Sheria zinazowapasa katika ulipwaji wa kodi.

Baraza hilo lilipata uwakilishi kutoka Tan Trade, TCCIA, NAKIETE, TRA, Twiga Cement na wafanyabiashara wakubwa na wadogo ambapo  walipata nafasi ya kuziainisha changamoto amabzo ni mkanganyiko wa Sheria za Biashara, mwingiliano wa Sheria na majukumu katika utekelezaji, kutokuwepo na uwazi katika taratibu za baadhi ya utekelezaji wa sera katika Biashara, ukiritimba katika kutekeleza Jambo pamoja na mazingira ya biashara kutokuwa rafiki.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya ya Kinondoni amewataka wafanyabiashara wadogo kukuza kipato chao  kwa kutumia njia sahihi ikiwemo uchukuaji wa mikopo isiyo na riba katika mkopo wa asilimia kumi kwa ajili ya wanawake, vijana na walemavu.


Imeandaliwa na

Kitengo Cha Habari na Uhusiano

Manispaa ya Kinondoni

Matangazo

  • UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU April 01, 2025
  • TANGAZO March 22, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 05, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA YA AFISA TEHAMA MSAIDIZI ULIOFANYIKA TAREHE 25/03/2024 March 25, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • ZAIDI YA MITI 1200 YAPANDWA KUADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU

    December 09, 2024
  • MAAMBUKIZI UKIMWI YAPUNGUA

    December 01, 2024
  • MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA KINONDONI

    November 29, 2024
  • WENYEVITI NA WAJUMBE WAPYA WAPEWA MAELEKEZO YA MAJUKUMU YAO

    November 28, 2024
  • Tazama zote

Picha Jongefu

IFAHAMU KATA YA MZIMUNI, MANISPAA YA KINONDONI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA MFUMO WA TAUSI
  • UJASIRIAMALI NA UTOAJI MIKOPO
  • MAKTABA YA PICHA
  • TAARIFA KWA UMMA
  • HOTUBA
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MIRADI ILIYOKAMILIKA

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • TOVUTI YA IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam

    Anuani ya Posta: S.L.P 31902

    Simu ya mezani: +255222170173

    Simu ya mkononi: +255733241052

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.