Thursday 2nd, January 2025
@Manispaa ya Kinondoni
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inatarajia kufanya Uzinduzi wa Uwekaji alama za utambuzi kwa kutumia hereni kwa Mifugo (Ng’ombe, Punda na Kondoo na Mbuzi) tarehe 26/09/2022 katika Kata ya Kinondoni Mtaa wa Ada Estate.
Hereni hizo zitawekwa alama maalumu za kielektroniki (barcode) ambayo itaweza kusomwa kwa kutumia kifaa maalumu na hivyo kutunza kumbukumbu sahihi za aina, idadi ya mifugo na taarifa nyingine muhimu zinazohusu mifugo.
Wizara ya Mifugona Uvuvi imetoa bei elekezi kama ifuatavyo: Ng’ombe na Punda ni kwa Tsh 1,750.00/ mnyama na Kondoo na Mbuzi ni Tsh 1,000.00/mnyama
Hivyo, Wafugaji wote mnatakiwa kufanya kuweka hereni mifugo yenu kushindwa kufanya hivyo, mifugo yako haitaruhusiwa kuuzwa minadani, kusafirishwa, kutolewa mahari au kuchinjwa machinjioni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.