Thursday 2nd, January 2025
@Viwanja vya shule ya msingi Bunju A, Kata ya Bunju
Siku ya kichaa cha mbwa duniani (World Rabies Day) huadhimishwa kila mwaka tarehe 28 Septemba, kwa lengo la kuhamasisha jamii kutokomeza ugonjwa wa kichaa cha mbwa kwa kufanya kampeni za chanjo na kutoa elimu kwa umma juu ya ugonjwa huu hatari. Kauli mbiu ya mwaka huu ni Afya moja: Bila vifo; "One Health: Zero Deaths".
Katika mwaka 2022 maadhimisho hayo yatafanyika katika viwanja vya shule ya msingi Bunju A katika Kata ya Bunju. Huduma mbalimbali zitatolewa zikiwemo utoaji wa chanjo kwa mbwa na paka dhidi ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa, kuogesha, utoaji wa dawa za minyoo, kukata kucha mbwa na matibabu kwa wanyama wagonjwa. Huduma zitatolewa bure.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Godwin Gondwe. Wananchi wote mnaalikwa kuleta mbwa na paka wapatiwe huduma siku hiyo.
Baada ya maadhimisho hayo zoezi hilo itaendelea kwa kila Kata kutoka tarehe 28 Septemba, 2022 hadi tarehe 7 Oktoba, 2022 hivyo Wafugaji mnatakiwa kupeleka mifugo yenu ofisi za Kata husika na gharama za za chanjo ni bure.
Kwa taarifa zaidi kuhusu maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya kichaa cha mbwa duniani, bonyeza hapa.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.