Wednesday 22nd, January 2025
@Dar es Salaam
Tanzania husherehekea maadhimisho ya Uhuru tarehe 9 Desemba kila mwaka. Katika siku hii mwaka 1961, Tanzania wakati huo Tanganyika ilipata uhuru kutoka kwa Uingereza.
Siku hiyo, Desemba 9, kulikuwa na fashifashi, shamrashamra na furaha jijini Dar es Salaam. Sherehe rasmi zilifanyika Uwanja wa Taifa na wakati huo huo kulikuwa na Mwenge wa Uhuru uliopelekwa kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro.
Kwa heshima ya mafanikio haya ya kihistoria, Serikali inafuatilia sekta zake kwa kutaja mafanikio yake, matatizo na changamoto ilizozikabili tangu Uhuru na kupanga mwelekeo wa baadaye. Mwaka 2021 Tanzania inaadhimisha miaka 60 ya Uhuru kwa kauli mbiu ya: "Tanzania imara, Kazi iendelee."
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.