Sunday 22nd, December 2024
@Viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere
Maonesho ya biashara yanayojulikana kama Saba Saba yalianza mwaka 1962 yakiwa ni maonesho ya Kilimo yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Wizara ya Biashara na Ushirika. Maonesho hayo yalikuwa na lengo la kukuza kilimo na ushirika.
Mwaka 1978 serikali iliunda Bodi ya Biashara ya nje kupitia sheria yake namba 5 ya mwaka huo, Bodi hiyo ilipewa mamlaka kushughulikia usafirishaji wa bidhaa za kitanzania nje ya nchi. Bodi ya Biashara ya nje ilipewa pia dhamana ya kukuza ushirikiano wa biashara ya kimataifa kupitia maonesho ya kibiashara, kufanya utafiti kuhusiana na biashara.
Miaka ya hivi karibuni maonesho hayo yamekuwa yakishirikisha nchi takribani 20 kutoka Kusini mwa Afrika (SADC) vilevile yamejulikana kama maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam na viwanja vinajulikana kama viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Tanzania ni Mahali Sahihi pa Biashara na Uwekezaji".
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.