Wednesday 15th, January 2025
@Dar es Salaam
Jiji la Dar es Salaam na JIji la Hamburg la nchini Ujerumani yataadhimisha miaka 12 ya uhusiano wa Miji Dada ulioanzishwa tarehe 01 Julai, 2010 baada ya Mamlaka za Majiji hayo kuridhia kuanzishwa kwa uhusiano huo.
Maadhimisho hayo yatafanyika kuanzia tarehe 30 Juni, 2022 hadi tarehe tarehe 03 Julai, 2022 ambapo pande zote mbili zitasheherekea mafanikio yaliyofikiwa hadi sasa katika utekelezaji wa miradi ya mabadiliko ya tabia nchi, afya, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, michezo na utamaduni, elimu, utalii, stadi za kazi za wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalum.
Kupitia uhusiano huo kumekuwa na fursa nyingi kwa Jiji la Dar es Salaam kufanya ziara za kujifunza na kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi katika Jiji la Hamburg na wenzao wa Hamburg pia kufanya ziara kama hizo katika Jiji la Dar es Salaam.
Manispaa ya Kinondoni kupitia ushirikiano huu na Jiji la Hamburg nchini Ujerumani wamefanikisha ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka na kuzalisha mbolea mboji katika Kata ya Mabwepande kwa fedha za kitanzania shilingi 5.56 bilioni.
Sherehe za maadhimisho ya uhusiano huo zitafanyika siku ya Jumapili, tarehe 03 Julai, 2022 katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam, hivyo wananchi wote wanakaribishwa kushiriki na kutumia fursa hiyo kwa manufaa ya Jiji la Dar es Salaam.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.