Sunday 22nd, December 2024
@KIGOGO-DOGODOGO CENTRE
Manispaa ya Kinondoni imekabidhiwa hati ya manunuzi ya jengo la kilichokuwa kituo cha kulelea watoto yatima (Dogodogo Centre) yenye thamani ya takribani shilingi milioni 400, kwa lengo la kubadilisha matumizi na kuwa kituo cha Afya.
Hati hiyo imekabidhiwa leo kwa Mstahiki Meya Manispaa ya Kinondoni Mh Benjamin Sitta ikishuhudiwa na kamati ya Fedha na Uongozi, pamoja na wananchi, hafla iliyofanyika katika Kata ya Kigogo, eneo lililopo jengo hilo.
Jengo la Dogodogo centre lililonunuliwa na Manispaa ya Kinondoni kwa ajili ya Kugeuzwa matumizi na Kuwa Zahanati.
Mganga Mkuu Manispaa ya Kinondoni Dr. Festo Dugange akieleza jambo kwa Mstahiki Meya wa Manispaa MH. Benjamini Sitta.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.