Idara ya Maji ni moja kati ya Idara zilizoko Katika Manispaa ya Kinondoni zenye majukumu yafuatayo:-
Huduma ya maji kwa wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, kwa kiasi kikubwa hutolewa na Mamlaka ya Maji ya Mjini Dar es Salaam (DAWASA) ambayo imekodisha shughuli za utoaji huduma kwa kampuni ya DAWASCO. Malengo ya Kitaifa ni kuwapatia wakazi wa Mijini maji kwa asilimia 90 ifikapo mwaka 2015 na asilimia 100% ifikapo 2025.
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inakadiliwa kuwa na wakazi wapatao milioni 929,681ambao hupata maji kutoka katika vyanzo vya mto Ruvu, pamoja na maji chini ya ardhi. Maji yanayozalishwa yanakidhi mahitaji kwa asilimia 73. Upungufu wa maji unasababishwa na uwezo mdogo wa vyanzo vya maji vya miradi ya maji ambayo ilijengwa mwaka 1940 na 1976 wakati huo idadi wa wakazi wa jiji ilikuwa ni ndogo. Maeneo yasiyohudumiwa na Mtandao wa DAWASA hupata maji kutoka Miradi inayoendeshwa na Taasisi, Sekta binafsi na Jumuiya za watumia maji, chanzo kikubwa cha maji haya ni visima virefu. Katika Manispaa yetu ya Kinondoni kuna visima 97 vinavyomilikiwa na Manispaa. Aidha kuna visima vya taasisi na watu binafsi visivyopungua 300 katika maeneo mbalimbali ya Manispaa.
Pamoja na juhudi za DAWASA, kuna miradi ya maji inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa Kinondoni kupitia mapato yake ya ndani ambayo ni Madale Kisauke, Boko Chama, Makongo Juu, Magomeni Dosi, Magomeni Idrisa, Msasani Makangira, Ndugumbi, Kigogo Mbuyuni, Mzimuni na Bunju shule na kupitia wadau mbalimbali wa maji ikiwemo; Programu ya maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RWSSP) Ujenzi wa mradi wa maji Mbuyuni Makongo ujenzi wake umekamilika, na visima vya Mbezi mtoni, Boko Dovya na Mabwepande na Miradi ya Tandale uliofadhiliwa na shirika la Belgium technical Corporation.
Halmashauri
|
Idadi ya visima
|
Idadi ya kamati
|
Idadi ya Jumuia
|
Idadi ya Wananchi
|
Idadi ya wananchi wanaopata huduma ya maji
|
|
|
Binafsi
|
Serikali
|
|
|
|
|
Kinondoni
|
301
|
97
|
93
|
4
|
929,681
|
660,074
|
MAHITAJI YA MAJI KWA SIKU KATIKA MANISPAA YA KINONDONI.
NA
|
MAHITAJI YA MAJI KWA SIKU (L)
|
MAJI YANAYOPATIKANA KWA SIKU (L/DAY)
|
|
UPUNGUFU KWA SIKU (L)
|
1
|
74,374,480.00
|
54,293,370
|
|
20,081,110
|
MIRADI ITAKAYOTEKELEZWA NA MANISPAA KATIKA MWAKA WA BAJETI 2016/17
NA
|
JINA LA MRADI
|
GHARAMA YA MRADI
|
CHANZO CHA FEDHA
|
1
|
Kumalizia mradi wa maji Makongo Mbuyuni
|
56,000,000.00
|
Mapato ya ndani
|
2
|
Kujenga kisima cha maji Mbopo
|
26,000,000.00
|
Mapato ya ndani
|
3
|
Kukarabati mradi wa maji Bustani ya Magomeni
|
25,000,000.00
|
Mapato ya ndani
|
4
|
Kufanya uchunguzi wa maji chini ya ardhi kuchimba na kuendeleza visima virefu viwili
|
60,000,000.00
|
CDG
|
5
|
Kuendeleza visima vya maji katika maeneo ya Mbopo, Kinondoni shamba, Mzimuni na changanyikeni
|
80,000,000.00
|
CDG
|
6
|
Kupanua mradi wa Maji Mabwepande mpaka Mbopo
|
55,280,000.00
|
World Bank
|
Na
|
MRADI
|
MAELEZO YA MRADI
|
HATUA YA UTEKELEZAJI HADI 30/9/2016
|
GHARAMA YA MRADI
|
1
|
UPANUZI WA MTAMBO WA RUVU CHINI (MCC)
|
Kupanua mtambo kutoka uwezo wa sasa wa mita za ujazo 196,000kwa siku hadi mita za ujazo 270,000 kwa siku ili kukidhi mahitaji ya maji hadi mwaka 2032.
|
Upanuzi umekamilika na Mtambo sasa unazalisha lita milioni 270 kwa siku kuanzia tarehe 23/3/2016.
|
|
2
|
UKARABATI NA UPANUZI WA MFUMO WA KUSAMBAZA MAJISAFI
|
Mradi utatekelezwa kupitia mkopo kutoka Benki ya Exim India. Kazi hii inahusu miradi ya mabomba madogo na makubwa pamoja na kuunganisha wateja kwenye eneo kati ya Mbezi hadi Kiluvya na Tegeta hadi Bagamoyo. Jumla ya Km 511.6 za mabomba na Jumla na matenki 4 yatajengwa katika maeneo ya Changanyikeni, Salasala, Wazo na Mabwe pande
|
Mkandarasi ameagiza asilimia 50 ya mabomba kutoka India, na amekamilisha upimaji wa njia za mabomba na mapitio ya usanifu wa mabomba na matenki, pamoja na mahitaji ya umeme wa pump za Booster Stations.
|
Dollar za Marekani milioni 32.927
|
3
|
UPANUZI WA MTAMBO WA RUVU JUU KUONGEZA UZALISHAJI MITA ZA UJAZO 114,000 KWA SIKU.
|
Kupanua mtambo kutoka uwezo wa sasa wa mita za ujazo 82,000 kwa siku hadi mita za ujazo 196,000 kwa siku ili kukidhi mahitaji ya maji hadi mwaka 2032
|
Katika mradi huu mabomba mapya yamelazwa ili kubadilisha yaliyopo ambayo yamechakaa na ambayo ni madogo kuweza kusafirisha maji yatakayoongezeka. Mabomba yaliyolazwa ni kama ifuatavyo; bomba jipya lenye kipenyo cha 1200 mm, 40km kutoka Mlandizi hadi Kibamba na bomba la 1000mm, 10km kutoka Kibamba hadi Kimara, kuendeleza bomba la 900mm, 19.1 km kutoka Tanita hadi Kibamba, pamoja na ujenzi wa tanki moja lenye jumla ya mita za ujazo 10,000 eneo la Kibamba, Ujenzi wa mradi umefikia 97%
|
224,145,528,100.00
|
4
|
MIRADI YA KUBORESHA NA KUPANUA MFUMO WA UONDOSHAJI MAJITAKA
|
Mchakato wa kutafuta mkandarasi utaanza baada ya kukamilisha usanifu na kupata fedha.
DAWASA inaendelea na kutafuta maeneo kwa ajili ya ujenzi wa mitambo mipya ya kusafisha majitaka itakayojengwa Jangwani, Kurasini na Mbezi Beach. |
Mchakato wa kumpata Mshauri atakayefanya mapitio ya usanifu na kutayarisha nyaraka za zabuni kwa ajili ya upanuzi wa mfumo wa majitaka umekamilika.
|
|
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.