KITENGO CHA BIASHARA
Kitengo cha Biashara ni Kitengo kilichopo chini ya Idara ya fedha na Biashara. Kitengo hiki kinalojukumu kubwa la kutoa leseni za biashara pamoja na leseni za vileo, na utoaji wa leseni hizi ni kwa mujibu wa sheria kama ifuatavyo:-
Leseni za biashara zinatolewa chini ya sheria ya leseni ya biashara Na. 25 ya mwaka 1972 na marekebisho yake ya 1980, 2013 kifungu 11(1) na marekebisho ya mwaka 2015.
Leseni za vileo zinatolewa chini ya sheria ya vileo ya mwaka 1968 kifungu Na. 28 na marekebisho yake ya mwaka 1981 na 2011.
Ushuru wa makazi unatozwa kwa kutumia sheria ya ulipaji wa Huduma za jiji Na. 23 (1972).
MAJUKUMU MENGINE NI KAMA HAYA YAFUATAYO:-
Kitengo cha Biashara pia kinayo majukumu mengine ambayo kinayatekeleza kama ifuatavyo;-
• Usimamizi na Ukaguzi wa nyumba za kulala wageni na
• Utozaji wa ushuru wa malazi (Hotel levy),
• Utoaji wa mafuzo na ushauri kwa wajasiriamali wadogo na wakubwa.
• Ukaguzi wa leseni zote na biashara,
• Ukaguzi wa Viwanda vidogo na vikubwa.
• Ushiriki na uandaaji wa maonyesho mbali mbali ya biashara.
• Usajili wa Pikipiki, Bajaji na Taxi.
• Kitengo cha Biashara kinahusika pia na Semina mbali mbali zinazotolewa kwa kushirkiana na taasisi mbali mbali za fedha ili kuwawezesha wajasiriamali kupata mikopo, Mfano; Banks, Finca, Pride, TBS n.k
TARATIBU ZA KUPATA LESENI.
Leseni zote za biashara hutolewa kwa kujaza fomu ya maombi Na TFN – 211. Mwombaji anatakiwa awe na umri wa miaka 18 au zaidi. Fomu yake ya maombi inatakiwa iambatishwe na nyaraka zifuatazo:-
• TIN
• TAX CLEARENCE
• MKATABA WA PANGO
• UTHIBITISHO WA URAIA (Kadi ya kura, cheti cha kuzaliwa, Passport).
• MEMORANDUM
• CHETICHA USAJILIWA JINA LA BIASHARA.
• CHETI CHA USAJILI WA MAKAMPUNI KAMA BIASHARA YAKO NI YA AINA HIYO.
• VYETI VYA UTAALAM KWA BAADHI YA BIASHARA.
• HATI YA KUISHI NCHINI KWA WAGENI KUTOKA NJE YA NCHI.
• VIAMBATISHO KUTOKA KWENYE TAASISI MBALI MBALI ZINAZOHUSISHWA NA AINA HIZO ZA LESENI KWA MFANO CRB, ERB, TFDA N.K
Dar es salaam, Tanzania
Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road
Namba za simu: +255 22 2170173
Namba ya simu :
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz