TEHAMA NA UHUSIANO.
Kitengo cha Teknolojia ya Habari Mawasiliano na Uhusiano (TEHAMA) kinajumuisha sehemu mbili ambazo ni
•Habari na Mahusiano
•Teknolojia ya Mawasiliano.
IDADI YA WATUMISHI.
Kitengo kinajumla ya watumishi 7
•Maafisa Habari wawili (2)
•Maafisa Tehama watano (5)
SEKTA YA HABARI NA MAHUSIANO.
•Katika sekta ya Habari na Mahusiano, kazi zinazotakiwa kufanyika ni
•Kusimamia Sera, mikakati na miongozo inayotolewa na Serikali kuu juu ya uendeshaji wa kazi za Habari na mahusiano.
•Kutoa ushauri wa kitaalam na huduma kwa Taasisi katika Nyanja za upashaji taarifa, mawasiliano na elimu kwa Umma.
•Kuandaa mpango, bajeti, mpango kazi na mpango mkakati wa kutekeleza kazi za Uhusiano katika Halmashauri.
•Kutangaza kazi na miradi inayofanyika katika Halmashauri.
•Kutangaza maeneo ya uwekezaji ya Halmashauri katika tovuti, Radio, majarida na njia nyinginezo za mawasilano.
•Kuhakisha Tovuti ya Halmashauri inataarifa mpya kila wakati pamoja na wasifu wa Halmashauri.
•Kuandaa na kutoa habari za Halmashauri katika machapisho.
•Kumshauri Mkurugenzi juu ya Mambo yanayohusiana na mawasilano, utoaji wa taarifa na uelimishaji kwa Umma juu ya majukumu yanayotekelezwa na Halmashauri ili kuimarisha mahusiano ya ndani na nje ya Taasisi
•Kushiriki katika mijadala ya jamii kuhusu masuala ya Halsmahauri.
•Kutumia TEHAMA katika kutoa elimu kwa jamii.
•Kusimamia press briefing za Halmashauri.
•Kuishauri Halmashauri juu ya uandaaji, uzalishaji na usambazaji wa nyaraka kwa wadau mbalimbali.
•Kutayarisha na kusambaza taaria mbalimbali kupitia vipeperushi, taarifa kupitia Makala mbalimbali kwenye vyombo vya habari kwa lengo la kuhamasisha na kuelimisha jamii juu ya majukumu ya taasisi
TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO
•Kutoa msaada wa kiufundi kwa watumiaji wa mfumo wa EPICOR, LGRCIS, LAWSON.GOT-HOMIS na POS.
•Marekebisho na matengenezo ya vifaa vya TEHAMA (Kompyuta, Printers na Scanners)
•Kuboresa daftari la Ki-electronic lenye kuonesha idadi na hali ya vifaa vyote vya TEHAMA. “General Inventory”
•Uboreshaji wa mapato kwa kutumia njia ya Kielectronic (POS MACHINE)
•Kurekebisha/kuthamini hitilafu zozote za mtandao wa kompyuta.
•Kuandaa “specifications” za vifaa vya TEHAMA
•Kurekebisha miundombinu ya mtandao.
Dar es salaam, Tanzania
Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road
Namba za simu: +255 22 2170173
Namba ya simu :
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz