MANISPAA YA KINONDONI YAZINDUA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI KWA KUFANYA USAFI KWENYE MASOKO.
Naibu Meya Manispaa ya Kinondoni Mh. George Manyama azindua siku ya maadhimisho ya Mazingira kwa kufanya usafi katika soko la Magomeni lililopo mkabala na Makao makuu ya Ofisi za Halmashauri hiyo jijini Dar Es Salaam.
Akiongoza zoezi hilo ambalo pia watendaji na wafanyabiashara wameshiriki amesema pamoja na kwamba ni siku ya Mazingira lakini swala la usafi liwe endelevu na lifanyike pia kwenye maeneo mengine,
Ametoa wito kwa wafanya biashara kuhakikisha wanaweka misingi na mikakati iliyo madhubuti ya kuhakikisha usafi unafanyika kwenye Masoko yao.
Naye Afisa Mazingira wa Manispaa hiyo Bw. Mohamed Msangi amewasihi wadau mbalimbali wa Mazingira kushirikiana na Halmashauri kwa kufanya usafi kwenye maeneo mbalimbali kuelekea kilele cha siku ya Mazingira duniani, tarehe 05/06/207.
Dar es salaam, Tanzania
Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road
Namba za simu: +255 22 2170173
Namba ya simu :
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz