Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni leo imeshiriki kikao kazi cha wataalam wa Mifugo na Kilimo kilichofanyika katika ukumbi wa JKT Mkoani morogoro.
Mkutano huo chini ya mwenyekiti wake Jaspar Mallya ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Mifugo Morogoro (LITA) umefanyika kwa lengo la kujadili maswala ya kiutendaji ya kilimo na mifugo pamoja na mstakabali mzima wa uratibu wa maonesho ya nane nane kwa mwaka 2017.
Mkutano huo pia umeshirikisha wataalam kutoka Kanda ya Mashariki yenye Mikoa minne ambayo ni Dar es Salaam, Morogoro, Pwani na Tanga.
Maonesho haya ya wakulima nane nane Kanda ya Mashariki yanafanyika katika viwanja vya nane nane Mkoani Morogoro kuanzia tarehe 01/08/2017.
Usikose kutembelea banda lá Manispaa ya Kinondoni uweze kujionea na kujifunza Kilimo cha faida cha mbogamboga.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
Dar es salaam, Tanzania
Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road
Namba za simu: +255 22 2170173
Namba ya simu :
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz