MATUKIO KATIKA PICHA
RAS Mkoa wa Morogoro Mh Clifford Tandari, leo amezuru katika banda la Manispaa ya Kinondoni na kujionea utaalamu mbalimbali kuhusiana na Kilimo, uvuvi na Mifugo.
Katika ziara yake aliyoambatana na Afisa Kilimo Bi. Rozalia Rwegasila amepata nafasi ya kutembelea mabanda ya wafugaji, wajasiriamali wadogowadogo pamoja na bustani za mbogamboga zilizooteshwa kitaalamu.
Kuelekea Nane nane 2017, yenye Kauli mbiu isemayo "Zalisha kwa tija mazao na bidhaa za Kilimo, mifugo na uvuvi, kufikia uchumi wa Kati", Kinondoni tunatekeleza.
Karibu Banda la Manispaa ya Kinondoni, uhabarike, uelimike kuhusiana na Kilimo na ufugaji wa Kitaalamu.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
Dar es salaam, Tanzania
Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road
Namba za simu: +255 22 2170173
Namba ya simu :
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz