NI KATIKA KUISIMAMIA NA KUITEKELEZA VEMA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI.
Kamati ya utekelezaji ya umoja wa vijana wa chama Cha mapinduzi (CCM)Mkoa wa Dar es salaam imeupongeza uongozi wa Manispaa ya Kinondoni kwa jinsi unavyosimamia na kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Ndg Mussa Kilakala imesema Manispaa hiyo niyakuigwa kwani imesimamia kikamilifu ilani kwa kuibua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuhakikisha inatekelezwa na kukamilika kwa wakati na ubora uliokusudiwa.
Kadhalika kamati hiyo pia imeshauri Halmashauri kuongeza utoaji elimu kwa vijana juu ya mikopo kwani ndio njia pekee ya wao kujishughulisha na ujasiriamali ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
Dar es salaam, Tanzania
Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road
Namba za simu: +255 22 2170173
Namba ya simu :
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz