• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
Kinondoni Municipal Council
Kinondoni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Wasifu wa Halmashauri
  • Utawala
    • Idara
      • Idara ya Utumishi
      • Afya na Usafishaji
      • Mipangomiji na Maendeleo ya Makazi
      • Kilimo na Mifugo
      • Elimu Sekondari
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • sheria
      • Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Tehama
    • Kata
      • Kinondoni
      • Magomeni
      • Makumbusho
      • Mwananyamala
      • Kijitonyama
      • Wazo
      • Bunju
      • Mbezi juu
      • Ndugumbi
      • Msasani
      • Kawe
      • Mzimuni
      • Mabwepande
      • Tandale
      • Kigogo
      • Mikocheni
      • Hananasif
      • Kunduchi
      • Makongo
      • Mbweni
    • Muundo wa utawala
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma zetu
    • Biashara
    • Elimu
    • Afya
    • Maji na Usafishaji
    • Ujasiriamali na utoaji wa mikopo
    • Ushauri katika Kilimo
    • Elimu ya ufugaji mifugo na nyuki
    • Vituo vya Ukusanyaji Mapato
  • Madiwani
    • Baraza la madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Vipeperushi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu za maombi
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

KINONDONI YA TUMIA BIL. 1.5 UJENZI WA MADARASA YA SHULE ZA MSINGI

Posted on: February 4th, 2020

WALIMU WASEMA MKURUGENZI KAGURUMJULI ANATEKELEZA IPASAVYO SERA YA ELIMU BILA MALIPO.

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imetumia kiasi cha shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi na ukaratabati wa vyumba 107 vya madarasa pamoja na matundu ya choo 157 kwa wanafunzi wa shule za msingi zilizopo katika Halmashauri hiyo.

Hayo yamebainisha na Afisa elimu msingi wa Halmashauri hiyo Kiduma Mageni wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya shule iliyokuwa na lengo la kuona maendeleo ya miradi hiyo ambayo inatekelezwa kwa kutumia Force Account.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa ziara hiyo, Ndugu Mageni amesema kuwa katika fedha hizo zilizotumika kujenga na kukarabati vyumba hivyo vya madarasa pamoja na matundu ya choo, shilingi milioni 771, 520,000 zinatokana na makusanyo ya ndani, shilingi milioni 455,140,000 ni pesa kutoka serikali kuu kupitia mpango wa EP4R.


Aidha Mageni ameongeza kuwa katika fedha hizo pia kiasi cha shilingi milioni 210, 004, 726 ni pesa kutoka mpango wa madarasa 100 ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Daniel Chongolo, na kiasi cha shilingi milioni 4, 140,000 nipesa zinazotokana na nguvu za wananchi.

Sambamba na hivyo, ndugu Mageni amebainisha madarasa yaliyojengwa ni 58, yaliyokarabatiwa ni 42  na kwamba kwa vyumba vilivyokarabatiwa vimeanza kutumika na wanafunzi huku vile vinavyojengwa vikiwa vimekamilika kwa asilimia 95.


Mageni amesema Halmashauri ya Kinondoni kupitia Mkurugenzi Aron Kagurumjuli pamoja na Mkuu wa Wilaya Mhe. Daniel Chongolo wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa inajenga na kukarabati madarasa hayo ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira mazuri.

Ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya tano inayo ongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli inatoa elimu bure na kwamba viongozi hao Mkurugenzi Kagurumjuli na Mkuuwa Wilaya Chongolo wanaitekeleza kikamilifu sera hiyo.


“ Niwapongeze sana kwa kazi nzuri wanayoifanya, tumejionea wenyewe wanafunzi wanakaa kwenye majengo mazuri,ya kisasa ,mengine bado yapo kwenye hatua ya mwisho kukamilika  na muda sio mrefu yatakabidhiwa ili watoto wetu  wa anze kuyatumia.

“Nampongeza sana  Mhe. Chongolo, Kagurumjuli na timu yake  yote wanafanya kazi kubwa, inaonekana, Rais wetu Dk. Magufuli ametoa elimu bure na sisi tunaitekeleza, nasio kwamba tunaishia hapa, bado tutaendelea kutekeleza zaidi na zaidi ili watoto wetu wasome kwenye majengo safi” amesema Mageni.

Mageni amesema ameridhishwa na ujenzi, ukarabati wa majengo hayo na hivyo kuwataka walimu hao kuwa wasimamizi wazuri wa miundombinu hiyo.

Kwa upande wa mwalimu hao waliokuwa katika ziara hiyo wamempongeza Mkurugenzi Kagurumli kwa kuwezesha ujenzi wa madarasa hayo na kwamba wanafunzi watasoma kwa nafasi.


Mmoja wa walimu hao ambaye ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mwenge, Janeth Mlenge alisema kuwa elimu bure inayotolewa na Rais Dk.Magufuli imetoa hamasa kwa wazazi na hivyo kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma.

Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Nyakasanga amesema kuwa kupitia mradi huo katika shule yake amejengewa vyumba nane vya madarasa  ofisi ya mwalimu mkuu  pamoja na matundu 13 ya choo na hivyo kumpongeza Mkurugenzi Kagurumjuli,Mhe. Chongolo kwa kuwapatia majengo hayo.

Hata hivyo walimu hao wameonyesha kufurahishwa na huduma hiyo ya kujengewa madarasa katika shule zao, sambamba na kukarabatiwa na kusema serikali kupitia Halmashauri ya Kinondoni inatekeleza vema sera ya Elimu bila malipo.


Imetolewa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano

 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Matangazo

  • TANGAZO KUHUSU VIBANDA VYA MWENGE February 22, 2021
  • TAARIFA KUHUSIANA NA WASTAAFU WANAOLIPWA NA HAZINA February 18, 2021
  • TANGAZO KUHUSU WAMILIKI WA KUMBI ZA BURUDANI, SHEREHE NA BAA January 22, 2021
  • HAWA HAPA WADAIWA SUGU WA LESENI ZA BIASHARA MANISPAA YA KINONDONI December 04, 2020
  • Tazama zote

Habari mpya

  • WATENDAJI WA KATA NA MITAA KINONDONI TIMIZENI WAJIBU WENU

    April 08, 2021
  • ZIARA YA KATA KWA KATA WILAYA YA KINONDONI YAANZA LEO

    April 01, 2021
  • MSTAHIKI MEYA MANISPAA YA KINONDONI MHE. SONGORO MNYONGE AKIFAFANUA JAMBO WAKATI WA BARAZA LA MADIWANI

    March 17, 2021
  • UWASILISHWAJI WA TAARIFA ZA KAMATI ZA KUDUMU-BARAZA LA MADIWANI.

    March 17, 2021
  • Tazama zote

Picha Jongefu

DCChongolo akemea vikali wakandarasi wazembe
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ilala Municipal website
  • Ubungo Municipal Council
  • Kigamboni Municipal
  • Temeke Municipal

Viunganishi Linganifu

  • TAMISEMI
  • eGoverment Agency
  • Manispaa ya Kinondoni yaongoza katika Makusanyo kufikia Dec.12,2017, 2017.
  • TUME YA UTUMISHI.Tangazo la nafasi za Kazi.

Idadi ya Wasomaji

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Dar es salaam, Tanzania

    Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road

    Namba za simu: +255 22 2170173

    Namba ya simu :

    Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti
    • Service

Hatimiliki