Hayo yalikuwa maneno ya Katibu tawala Mkoa wa Dar Es Salaam Bi Theresia Mmbando, alipozuru katika banda la Kinondoni kwenye maonesho ya Nane nane yanayoendelea Mkoani Morogoro viwanja vya Tungi.
Alipokuwa banda hilo alipata nafasi ya kutembelea vikundi vya wajasiriamali wadogowadogo wanaojishughulisha na usindikaji wa vyakula kutokana na mazao yanayozalishwa, watengeneza mivinyo, wafugaji wa kuku, mbuzi Ngombe, sungura na njiwa.
Halikadhalika ametembelea bustani za mbogamboga, na kujionea utaalamu uliopo wa kutumia mifuko na kuitandaza ardhini, utaalamu wa kutumia Net House(green house) kwa lengo la kuzuia wadudu, na tekinolojia ya Hydroponic fodder.
Ni Kinondoni pekee utapata utaalamu huu kuelekea kilele cha Nane nane na kauli mbiu isemayo "Zalisha kwa tija bidhaa na mazao ya Kilimo, mifugo, na uvuvi kuelekea uchumi wa Kati".
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
Dar es salaam, Tanzania
Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road
Namba za simu: +255 22 2170173
Namba ya simu :
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz